April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM: Kwanini elimu ya Muungano isitolewe?

Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum (CCM),

Spread the love

RITTA Kabati, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), ametaka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuona uwezekano wa kupeleka elimu ya muungano kwa ngazi ya kata na wilaya badala ya kufanya maadhimisho hayo kitaifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kabati ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Aprili 2019 bungeni alipouliza swali la nyongeza. Alitaka kujua, ni lini serikali itaona umuhimu wa kutoa elimu ya muungano kwa vijana kwa ngazi ya vijiji, mitaa badala ya kufanya maadhimisho ya muungano kitaifa.

“Kwa kuwa vijana wengi hawajiu masuala ya muungano, na kumekuwepo na maadhimisho ya muungano kitaifa, ni kwanini sasa elimu isiwe inatolewa kwa ngazi za chini ili vijana wengi waweze kujifunza vyema historia ya muungano badala ya kufanya maadhinisho hayo kitaifa?” amehoji Kabati.

Awali katika swali la msingi, Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) alitaka kujua ni kwanini sherehe za muungano zimekuwa zikifanyika na kupewa nafasi kubwa kitaifa tu.

Akijibu swali hilo la nyongeza Januari Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amesema kuwa, pamoja na sherehe hizo kufanyika kitaifa, bado elimu juu ya muungano inaendelea kufundishwa.

Amesema, kwa kutuumia vyombo mbalimbali vya habari, wizara imekuwa ikitoa elimu ya muungano ili kuhakikisha muungano unadumishwa.

Mussa Sima, Naibu Waziri wa wizara hiyo amesema kuwa, sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huadhimishwa kwa kuzingatia muungozo wa maadhimisho na sherehe za kitaifa kwa mwaka wa 2011, uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndiyo inadhamana ya kuratibu sherehe zote za kitaifa.

“Aidha, katika mwongozo huo sura ya tano katika maelezo ya utangulizi imeelezwa kuwa, sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitafanyika 26 Aprili kila mwaka katika uwanja wa mpira jijini Dar es saalam, mahali ambapo udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa.

“Sherehe hizo zinaweza kufanyika nje ya Dar es Salaam kama kamati ya maadhimisho na sherehe za kitaifa zitakavyoelekeza” alisema Sima.

Sima alisema serikali itaendelea kuzingatia muongozo huo wa maadhimisho ya sherehe za kitaifa hadi hapo itakapokuwa na sababu za msingi zitakazofanya muongozo huo ufanyiwe marekebisho kwa niaba ya kuuboresha.

Kutokana na hilo alisema serikali inahimiza wananchi kuadhimisha sherehe hizo kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo Usafi, michezo, makongamano na shughuli mbalimbali za maendeleo.

error: Content is protected !!