Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Mbunge CCM awapigania wagonjwa wa saratani, figo bungeni
AfyaHabari za Siasa

Mbunge CCM awapigania wagonjwa wa saratani, figo bungeni

Hospitali ya magonjwa ya Kansa ya Ocean Road
Spread the love

RITTA Kabati, Mbunge Viti Maalumu mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ameiomba Serikali kuwapunguzia gharama za matibabu wagonjwa wa saratani na figo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kabati ametoa ombi hilo leo Alhamisi tarehe 11 Juni 2020, bungeni jijini Dodoma, wakati akihoji Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzia gharama wagonjwa hao, hasa gharama za malazi kwa wagonjwa wanaotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam.

Wagonjwa wa saratani wanatibiwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, ambapo hospitali hiyo ni maalumu kwa ajili ya kutoa matibabu kwa wagonjwa hao.

Kabati ameishauri Serikali kujenga jengo maalumu la makazi ya wagonjwa wa Saratani na Figo, kwa kuwa matibabu yao huchukua muda mrefu.

“Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzia gharama za malazi wagonjwa wa saratani na figo wanaotoka nje ya Dar es Salaam kwa kuwajengea jengo maalum la makazi kwa kuwa matibabu yao huchukua muda mrefu na kwa kuwa maradhi yanayowasumbua siyo rahisi kwao kutembea umbali mrefu?” amehoji Kabati.

Akijibu swali hilo kwa njia ya mtandao wa Bunge, Waziri wa Afya amesema changamoto hiyo inayowapata wagonjwa wanaopata nafuu na kutolazimika kulala hospitali, hasa wale wagonjwa wa Saratani.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Waziri wa Afya amesema, Serikali imeamua kujenga hosteli kwa ajili ya wagonjwa wa aina hiyo ambapo watapewa huduma ya malazi bila malipo.

Amesema mpango wa ujenzi wa hosteli hizo umeanishwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020.

Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum Iringa (CCM)

“Pamoja na jitihada zote hizo, wamekuwepo wagonjwa ambao hupata nafuu na kutolazimika kulala hospitali, Serikali imeamua kujenga hosteli kwa ajili ya wagonjwa wa namna hiyo pamoja na wale wanaoruhusiwa kutoka wodini ikiwa bado wanahitajika kufuatilia matibabu yao,” amejibu Waziri wa Afya.

Kuhusu wagonjwa figo, Waziri wa Afya amesema Serikali inawapatia sehemu za kulala wagonjwa wanaotakiwa kubaki hospitali.

“Wagonjwa wanaopatiwa huduma za usafishaji wa figo (dialysis), huwa hawakai muda mrefu Hospitali, bali matibabu yao yanaweza kuwa ni ya mara kwa mara. Serikali inawapatia wagonjwa hawa sehemu ya kulala na wanaoweza kurudi majumbani huruhusiwa,”amesema Waziri wa Afya na kuongeza:

“Suluhisho la mwisho la wagonjwa wanaopatiwa huduma ya Dialysis, ni kupatikana kwa figo kwa ajili ya upandikizaji wa figo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!