June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM atangaza kujizulu

Spread the love

 

SHEHA Mpemba Faki, Mbunge mteule wa Konde Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni siku 15, tangu alipotangazwa mshindi wa nafasi hiyo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Faki aliibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo ulioshirikisha vyama 12 ambao uliofanyika Jumapili ya tarehe 18 Julai 2021.

Uchaguzi huo, ulifanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Pemba, Khatibu Said Haji wa ACT-Wazalendo kilichotokea tarehe 20 Mei 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Taarifa ya Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliyoitoa leo Jumatatu, tarehe 2 Agosti 2021 imesema, “Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko barua ya kujizulu kwa mbunge mteule Sheka Mpemba Faki.”

Shaka amesema, katika barua hiyo, Faki ameeleza amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia, jambo ambalo chama hakina uwezo wa kumzuia, hasa ikizingatiwa kwamba ni haki ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM.

“Chama Cha Mapinduzi, kinawaomba wanachama wote kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati tunasubiri taratibu nyingine,” imeeleza taarifa hiyo ya CCM

error: Content is protected !!