June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ataka zigo la kodi lihamishwe kwa wabunge

Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Slaa

Spread the love

 

Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Slaa, ameshauri wabunge wakatwe kodi katika mishahara yao, ili wachangie maendeleo ya nchi, kama wananchi wanavyochangia kupitia tozo za miamala ya simu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Slaa ametoa ushauri huo jana tarehe 22 Julai 2021, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzinga, jijini Dar es Salaam.

“Ni wakati muafaka sisi wabunge tulipe kodi, ili tupate uwezo wa kusimama mbele ya watu kuwaambia walipe kodi. Na sisi tuanze kulipa kodi kwenye mishahara yetu,” alisema Slaa.

Slaa alisema, kama wabunge watakatwa kodi, italeta usawa kati wigo wa ulipaji kodi.

“Hakuna sababu ya kuwa na wengine hawalipi, ukishakuwa haulipi unakosa nguvu ya kuwaambia wengine walipe,” alisema Slaa.

Tozo hizo zinazotozwa katika miamala ya simu, zilianza kutumika kuanzia tarehe 15 Julai mwaka huu.

Ambapo Serikali inatoza kuanzia Sh. 10 hadi 10,000, katika muamala wa kutuma au kutoa pesa, kulingana na thamani ya muamala wa fedha husika.

error: Content is protected !!