May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ashauri taasisi huru ziundwe kuidhibiti Serikali

Mbunge Viti Maalum mkoani Tanga (CCM), Mhandisi Mwanaisha Ulenge

Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalum mkoani Tanga (CCM), Mhandisi Mwanaisha Ulenge, amesema kuna haja ya nchi kuwa na taasisi huru, iitakayodhibiti utendaji wa wizara na taasisi za umma. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Ulenge ametoa ushauri huo leo Alhamisi tarehe 27 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo, kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mbunge huyo viti maalum amesema, utaratibu wa sasa wa wizara hizo kujitathimini zenyewe, hasa Wizara ya Fedha na Mipango, hauwezi kudhibiti utendaji wa Serikali.

“Waziri mkuu kuna idara za Serikali Kuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, zimekuwa zikitekeleza mipango yake, wakati huo huo zinajifanyia tathmini zenyewe. Mfano hai Wizara ya Fedha na Mipango, imekuwa na kitengo cha tathmini ndani ya wizara,” amesema Ulenge na kuongeza:

“Iili tuweze kuidhibiti na kuisimamia Serikali ipasavyo, hatuoni haja ya kuwa na taasisi inayojitegemea ya kuisimamia Serikali, kufanya tahimini na kutunga mifumo ya ufuatiliaji nchini?”

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Akijibu ushauri huo, Waziri Majaliwa amesema hakuna haja ya uundwaji wa taasisi hiyo, kwani Serikali imeweka utaratibu wa wizara kujifanyia tathimini, ambao hukagua utendaji wake na wa taasisi za umma.

Hata hivyo, Waziri Majaliwa amesema Serikali itaboresha mifumo ya ufuatiliaji wizara hizo.

“Lakini nalichukua hilo wazo, baadae nitakupa majibu kwa namna nyingine, ili uweze kupata uelewa mpana juu ya wajibu huo na kama kuna udhaifu, tutaangalia na tutaenda kuboresha. Lakini suala la mipango na tathimini, liko katika kila sekta,” amesema Majaliwa.

error: Content is protected !!