January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM asafiria nyota ya Magufuli

Rais John Magufuli

Spread the love

MGOMBEA ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Dodoma Mjini, Dk. David Malole, ametumia kigezo cha kusoma shule moja na mgombea urais kupitia chama hicho Dk. John Magufuli kuomba kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kutetea nafasi hiyo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Dk. Mallole alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati alipokuwa akijinadi mbele ya wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Nala iliyopo wilaya ya Dodoma mjini.

Amesema kwa sababu amesoma shule moja ya seminari na mgombea wa Urais, Dk. Magufuli anaamini watawaletea maendeleo watanzania likiwemo Jimbo la Dodoma Mjini.

Mbali na hilo aliwatumainisha wananchi wa jimbo la Dodoma mjini kuwa iwapo atachaguliwa tena kuna uwezekano mkubwa wa kupatiwa nafasi mbalimbali ya uongozi ndani ya serikali jambo ambalo litachochea maendeleo katika jimbo hilo.

“Magufuli ni rafiki yangu sana na ananipenda sana kwa sababu nimesoma naye shule moja ya seminari, naimani kwa kushirikiana naye tutawaletea maendeleo,” amesema.

Kuhusu Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), alisema mpaka sasa ameweza kurudisha Manispaa kata saba ambazo zilikuwa zinamilikiwa na CDA.

Nae, Antony Mavunde alikuja na kauli mbiu yake kuwa “umaskini wa watu wetu na ukosefu wa ajira.” amesema.

Aliifafanua kauli mbiu hiyo kuwa lengo ni kuhakikisha umaskini uliopo mkoani Dodoma utoa kwa kutoa ajira kwa vijana kama alivyofanya katika wilaya ya Mpwapwa.

“Makaburi yanafutika kutokana na alama, lakini wema haufutiki unabaki moyoni…nipeni ubunge ili niwatatulie matatizo yenu,” amesema Mavunde ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.

Naye, Emmanuel Kamara amesema atashughulikia masuala mawili ikiwa ni pamoja na maji na kituo cha afya.

“Nyie si mna macho mbona mnaambiwa sera zisizotekelezeka na nyinyi mnakubali…mimi sina lugha ya kuwapaka asali bali nitawasaidia katika matatizo yenu, naombeni kura zenu ya kuwa mkali katika maendeleo yenu,” amesema.

Kwa upande wake, Haidary Gulamali amesema atashughulika na suala la uchumi kwa sababu ni mfanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuleta gari la kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji.

Pia, aliwaahidi wananchi hao kutochukua hata shilingi ya mshahara wake wala marupurupu hivyo atazipeleka kwenye mfuko wa Jimbo.

Naye, Mohammed Mgoli amesema iwapo atachaguliwa atakaa kikao na wananchi wake na kuorodhesha matatizo yaliyopo.

“Sitakaa mjini kabisa nitakaa na nyinyi ili tuweze kutatua matatizo yaliopo kwa sababu mjini hapakaliki kabisa,” alisema na kuongeza kwamba: “Nipeni kura mimi mlalahoi mwenzenu ili nije tusaidiane huu ulalahoi tujikwamue katika maisha magumu.”

Mgombea Alexander Muruke amesema iwapo atachaguliwa anaweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika Jimbo la Dodoma mjini.

Kwa upande wake, Mussa Luhamo amesema iwapo atachaguliwa atahakikisha anaisimamia serikali katika mambo ya msingi.

Nae, Robert Mtyani aliwataka wakina mama kumchagua kwa sababu ana mambo ya msingi kwa ajili yao.

Mgombea Stevin Masangia, amesema atatumia vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma kutoa elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia wananchi kujikomboa kiuchumi.

Nae, Antony Kanyama amesema kama atapewa nafasi ya kuwa mbunge atasimamia kina mama wapate mikopo hasa waliombali na manispaa.

“Nitasimamia suala la elimu kwa kuhakikisha mnapa elimu sahihi na kwa wakati.”

“Wakati mwingine roho inaniuma unakuta mfugaji kakonda kuliko hata ngombe wake mimi nitawasaidia mfuge kwa kisasa,” amesema.

Hata hivyo, wananchi hao walipata nafasi ya kuuliza maswali na wengi wao wakitaka kutatuliwa tatizo la maji, barabara, ardhi na vituo vya afya huku tatizo kubwa lililokuwa likilalamikiwa ni CDA.

error: Content is protected !!