May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM aomba hospitali, serikali yamjibu

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

JAFARI Chege, Mbunge wa Rorya (CCM), mkoani Mara, amehoji serikali lini itakipandisha hadhi kituo cha afya Kinesi kinachohudumia vijiji 27 ili kiwe hospitali. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Chege amehoji suala hilo, leo Alhamisi, tarehe 28 April 2021, Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Je, ni lini Kituo cha Afya Kinesi kitapandishwa hadhi na kuwa Hospitali kamili
kutokana na Kituo hicho kuhudumia wananchi zaidi ya Vijiji 27 katika Jimbo la Rorya,” amehoji Chege

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Tamisemi-David Silinde amesema, ili kuboresha huduma za afya katika wilaya ya Rorya Sh.1.5 bilioni zimetolewa kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa hospitali ya halmashauri.

Amesema, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imetenga Sh.500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu na Sh.500 milioni, imetolewa kwa ajili ya vifaa vya tiba.

Silinde amesema, “Serikali haitakipandisha hadhi kituo cha afya Kinesi kwa kuwa, bado kinaendelea na ujenzi huo.”

error: Content is protected !!