January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM amwaga ahadi akiwania uspika

Spread the love

 

MBUNGE wa Mlimba (CCM), Mkoa wa Morogoro, Godwin Kunambi amechukua fomu za kuwania kurithi mikoba ya Job Ndugai ya uspika wa Bunge la Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kunambi amechukua fomu hiyo Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumatatu, tarehe 10 Januari 2022 akisema ana uzoefu wa kutosha kuongoza muhimili huo wa Bunge.

“Nimesukumwa na hali ya kutimiza haja yangu ya msingi, nina sifa za kuwa Spika wa Bunge la Tanzania,” amesema

Kunambi amesema, “nimehudumu kama mwanasheria wa CCM kwa miaka mitano. Nimehudumu kama mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kilana nimejipima sifa na uwezo ninao.”

“Ninawaahidi wabunge kwamba nitakwenda kusimamia uhuru na usawa kwa wabunge wote.”

Kunambi anaungana na Mbunge wa zamani wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho cha uspika ambapo fumo zimeanza kutolewa leo hadi 15 Januari 2022.

Mchakato huo umetangazwa baada ya Job Ndugai kutangaza kujizulu nafasi hiyo wiki iliyopita.

error: Content is protected !!