October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM amvimbia Spika Ndugai

Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesimamisha uwakilishi wa Mbunge wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele hadi Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo tarehe 16 Mei 2019, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema, Bunge limechukua hatua hiyo baada ya kudai Masele amekuwa akigonganisha mihimili miwili (Serikali na Bunge).

Amesema, mbunge huyo licha ya kuitwa, amekaidi wito wake wa kuja katika kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Spika Ndugai amesema, Jumatatu ya tarehe 13 Mei 2019 alimuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Masele katika Bunge lake.

“Baada ya kumuandikia arudi nyumbani ili aje ahudhurie Kikao cha Kamati ya Maadili, amekuwa akihutubia lile bunge akisema japo ameitwa lakini ameambiwa na waziri mkuu a ‘disregard’ (kaidi) wito wa spika aendelee na mambo yake kule.

“Kitu ambacho ni uongo na kimedhalilisha nchi, ni kiongozi anayefanya mambo ya hovyo hovyo na ndio maana tumemuita kidogo kwenye Kamati ya Madili atufafanulie,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai amesema, wamesitisha uwakilishi wa Masele hadi pale Kamati ya Maadili ya Bunge na ya CCM itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

https://www.youtube.com/watch?v=olENoPMY-Io

“Sasa kwa kuwa tumeuita tangu Jumatatu hataki kurudi, nimemuandikia barua rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi tuliompatia Masele katika Bunge la PAP hadi hapo kamati ya maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.  kwa muda Masele hatokuwa mbunge hadi tutakapomalizana naye hapa,” amesema.

Spika Ndugai amesema, Masele ameitwa kuhojiwa kutokana na kutoridhidhwa na mwenendo wake, akidai kwamba anafanya mambo ya hatari ikiwemo kugonganisha mihimili ya nchi.

Spika Ndugai amesema, Masele anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu ikiwemo kukaidi wito wake pamoja na kupeleka taarifa za uongo serikalini.

“Kwa mtazamo yetu amekuwa akifanya mambo ya hatari kubwa, ikiwemo kugonganisha mhimili, anapeleka kwenye mhimili wa serikali juu kabisa maneno mengi ya uongo ushahidi hupo, na kulidhalilisha bunge.

“Ni kiongozi amejisahau, hajui anatafuta kitu gani, sisi tunamuita kwa ajili ya mambo ya hapa nyumbani kwa utovu wa nidhamu,” amesema Spika Ndugai.

error: Content is protected !!