January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM akikaba Serikali yake

Spread the love

MBUNGE wa Busokelo, Fredy Mwakibete (CCM) ameitaka serikali kuona umuhimu wa kutengeneza barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa km 82 kwa kiwango cha lami kutokana na kuwa mbovu kwa muda mrefu sasa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza swali na kutaka kujua serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kilometa 72 zilizobaki.

“Kwa muda mrefu wananchi wa Busoke wamekuwa wakikumbana na adha kubwa ya ubovu wa barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa kilometa 82 inayoanzia Katumba (RDC) kupitia Mpombo, Kadete, Isange, Lwangwa, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) ambapo barabara hiyo imekuwa katika mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami kwa muda mrefu na mkandarasi huyo eneo la ujenzi kwa kipande cha kilometa 10.

“Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami cha kilometa 72 zilizobaki,” amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Edwin Ngonyani na amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo katika mwaka wa fedha 2009/10 serikali kupitia wakala wa barabara ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ambapo upembuzi yakinifu na na usanifu wa kina umekamilika mwezi Februari 2012.

Amesema baada ya usanifu wa kina kukamilika 2013/14 kiasi cha fedha Sh. 1,270 milioni kilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 2.5 kwa kiwango cha lami.

Amesema serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi Aprili 2014 wakala wa barabara aliingia mkataba na kampuni ya CICO kujenga kilometa 10 kuanzia Lupaso hadi Bujesi (Wilaya ya Busokelo) kwa gharama ya Sh. 8,929.724 milioni.

error: Content is protected !!