May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM aivimbia serikali

Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

Spread the love

 

NICODEMUS Maganga, Mbunge wa Mbogwe kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM), amegomea majibu ya serikali, kwamba jimboni kwake serikali imechimba visima virefu vya maji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mganga alipinga majibu hayo baada ya Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji leo tarehe 14 Aprili 2021, kusema serikali imechimba visima 26 jimboni humo na kuwa, vinatumika mpaka sasa.

“Sijaridhishwa na majibu ya serikali, hivyo visima vimechimbwa wapi?” amehoji Manga na kuongeza “mimi ni mbunge wa Mbogwe na ninaishi huko, lakini sijawahi kuona hayo maji naomba kujua visima viko wapi?”

Mbunge huyo amelieleza Bunge, kwamba wananchi wake wanaendelea kuteseka kwa adha ya maji, akisitiza majibu ya waziri huyo ni ya kwenye makaratasi.

Hata hivyo, Waziri Mahundi ameahidi kuongozana na mbunge huyo jimboni kwake, ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kutumia maji ya Ziwa Victoria kukabili shida hiyo ya maji.

error: Content is protected !!