Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM ‘aichana’ serikali
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge CCM ‘aichana’ serikali

Spread the love
JOSEPH Msukuma, Mbunge wa Shinyanga Vijijini amesema, serikali imekuwa ikiwekeza mabilioni ya fedha katika miradi ambayo haina faida kwa Taifa. Anaripoti Mwamdishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Februari 2021, wakati akijadili Mpango wa Taifa 2021/2022 akisisitiza, Watanzania hawaoni faida ya miradi hiyo.

“Katika kipindi kilichopita, serikali imekuwa na mradi mkubwa, ya mabilioni ya pesa ambayo haina impact (matokeo) yoyote kwenye Taifa.

“Watanzania wachapakazi hasa wale wa chini, hatuoni faida ya miradi mkubwa ambayo serikali imewekeza mabilioni ya fedha,” amesema Msukuma.

Ametolea mfano mradi wa nyumba za Morocco, Soko la Morogoro, Jengo la Machinga na Soko la Ndugai kwamba mabilioni yametumika lakini hakuna matokeo.

“Mnashindwa kutafakari kwamba mnapojenga masoko, mnapojenga mastendi makubwa ya mabilioni, ile ni huduma. Sasa nyie mnaviweka kama vitega uchumi na watu mnaowawekea vitega uchumi ni masikini, mama ntilie.

“Ushauri wangu, pesa hizi ambazo tunawekeza kwenye mavitu ambayo hayazalishi, tungeziwekeza kwa watu wa chini kwa mfano; tukichukua haya mabilioni halmashauri ikaandika miradi, … tukaenda kuboresha mabarabara yetu vijijini, wakulima watalima vizuri mazao yao yatasafirishwa kwa bei nafuu, itakuwa na impact (matokeo) kwenu walaji, mtapata kwa bei ndogo,” amesema.

Pia amewataka wabunge wenzake kueleza ukweli kwamba, mtaani hali ni mbaya.

“Nataka kushauri kuhusiana na suala la biashara mitaani. Tusioneane aibu wala tusifichane, ukweli hali ni mbaya. Watu wanafunga maduka.

“Watu wamekatika mitaji lakini sioni namna ambayo serikali yetu na viongozi wetu labda mnakuja na mawazo mbadala ya kuweza kuona namna gani kuwabeba hawa wafanyabiashara,” amesema.

Mbunge huyo eleza kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya kipindi cha sasa cha Rais Magufuli na tawala zilizopita akieleza, tawala zilizopita kulikuwa na afueni katika ufanyaji biashara.

Na kwamba, mawaziri wamekuwa wakimuogopa rais kumwambia ukweli hivyo, amemwomba Rais Magufuli kukutana na wafanyabiashara.

“Ni kweli maduka yanafungwa, wala tusifichane na kwanini yanafungwa, tuone namna ya kuzibadilisha sheria. Wafanyabiashara wale waliopo humu, enzi za nyuma kabla ya serikali ya awamu ya tano, ilikuwa inaweezekana ukakamatwa ukapiga faini ukalipa, ilikuwa inawezekana kujadili.

“Kwenye hiki kipengele naona mawaziri wanamuogopa mheshimiwa rais, sasa kwa sababu sisi wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwenye maeneo yetu tulikotoka, nimuombea rais awaite wafanyabiashara. Tukiendelea kufumbiana macho, watu wanaendelea kufilisika,” amesema Msukuma.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!