Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM ahojiwa kwa ‘kugawa’ rushwa
Habari za Siasa

Mbunge CCM ahojiwa kwa ‘kugawa’ rushwa

Spread the love

TAASISI ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemuhoji Lingstone Lusinde, aliyekuwa Mbunge wa Mtera (CCM) kwa tuhuma za kugwa rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kwa mujibu wa Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma, Lusinde alifikishwa katika ofisi za taasisi hiyo zilizoko wilayani Chamwino, Jumatano tarehe 8 Julai 2020.

Kibwengo amesema, Takukuru ilimuita na kumuhoji Lusinde, baada ya kupata taarifa ya kwamba, wajumbe wa vikao vya uteuzi wa wagombea wa CCM nyumbani kwake, kwa minajili ya kuwapa fedha kama kishawishi ili wampitishe kugombea katika uchaguzi huo.

Kibwengo amesema, baada ya mwanasiasa huyo kuhojiwa, aliachiwa na kuwamba uchunguzi juu ya sakata hilo unaendelea.

“Tulipata taarifa ya kwamba anakusanya wapigakura nyumbani kwake awapatie fedha kama kishawishi. Jana tulimhoji ofisini kwetu Chamwino, na kisha tuliamuachia. Lakini uchunguzi unaendelea,” amesema Kibwengo.

Lusinde alikuwa mbunge wa Mtera kwa vipindi viwili mfululizo, kuanzia mwaka 2010-2015 hadi 2015-2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!