December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ahoji utatuzi tatizo la maji

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Azza Hamad (CCM) ameitaka serikali iweke wazi ni lini itatatua tatizo la maji katika maeneo mbalimbali nchini. Anaandika Danny Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo amesema suala la ukosefu wa majini nchini limekuwa kero licha ya kuwepo kwa vyanzo vingi vya upatikanaji wa maji.

Kauli hiyo ameitoa leo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kuitaka serikali ieleze ni hatua gani ambazo zinachukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo la maji linaisha.

Kwa upande wake Mbunge wa Mombo, David Silinde (Chadema) katika swali la nyongeza alitaka kujua serikali inatekelezaje sera ya maji ya mwaka 2002 ambayo inamtaka kila mtu kupata maji kwa kwa mita 40 toka alipo.

“Sera ya maji ya mwaka 2002 inamtaka kila mtanzania kupata maji kwa ubali usiopungua mita 40 lakini kwa sasa bado tatizo hilo ni kubwa, je serikali imejipangaje kumaliza tatizo hilo,” alihoji Silinde.

Awali katika swali la msingi la Mbunge Azza alitaka kujua mradi wa maji wa kisima kirefu katika mji mdogo wa Tinde ambao umechukua muda mrefu utakamilika lini.

Akijibu mawali hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemai), Selemani Jafo mesema serikali inajipanga kuhakikisha inamaliza adha kubwa ya maji ambayo inawakumba Watanzania walio wengi.

Amesema ni kweli tatizo la maji ni kilio cha wabunge wengi lakini kutokana na ukusanyaji wa mapato katika serikali ya awamu ya tano tatizo hilo litakuwa historia.

error: Content is protected !!