Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM ahoji ahadi za serikali
Habari za Siasa

Mbunge CCM ahoji ahadi za serikali

Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM)
Spread the love

CATHERINE Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) leo tarehe 16 Aprili 2019, ameitaka serikali kueleza ni lini itakamilisha ahadi zake ilizotoa kwa jamii? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akiuliza swali la nyongeza bungeni, Catherine amehoji ni lini serikali itaweza kukamilisha ahadi zake hususani katika ujenzi wa soko la Mto wa Mbu, Arusha.

“Serikali imekuwa ikitoa ahadi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, lakini ahadi hizo zimekuwa zikichelewa. Mfano ni ahadi ya ujenzi wa soko la mto wa mbu mkoani Arusha, je ni lini ahadi ya ujenzi wa soko itakamilika?” amehoji Catherine.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Segerea, Bonnah Kamol (CCM) alitaka kujua ni kwanini serikali isijenge soko kubwa mbadala linaloweza kufikiwa na wananchi wa Kata ya Kinyerezi, Bonyokwe, Segerea na kata nyingine.

Pia mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini soko la Kinyerezi lililozinduliwa na Mwenge mwaka 2017, lisifunguliwe ili kutoa huduma kwa wananchi wanaolizunguka?

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri was Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI- Mwita Waitara amesema kuwa, serikali inatambua ahadi zake zote na itazitekeleza.

“Serikali inatambua ahadi zote na zitatekelezwa kuhusu ujenzi wa soko la mto wa mbu mkoani Arusha, kutokana na hali hiyo, fedha za ujenzi wa soko zipo ni pamoja na kutoa wataalamu wa ujenzi wa soko hilo,” amesema Mwita.

Mbali na hilo alisema kuwa halmashauri ya Manispaa ya Impala iliweka kipaumbele cha kutekeleza Mardi wa kimkakati wa ujenzi wa soko la kisutu utakao gharimu kiasi cha sh.bilioni 12.17 na hadi sasa mradi umepokea sh.bilioni 3.92 na ujenzi unaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!