November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ahoji ahadi ya Hayati Magufuli, ajibiwa

Prof. Patrick Ndakindemi. Mbunge wa Moshi vijijini

Spread the love

 

SERIKALI imepanga kuendeleza ujenzi na matengenezo ya barabara nchini ikiwemo Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, kadri ya upatikanaji wa fedha. anaripoti Jemima Samwel DMC…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 27 Aprili 2021 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde, wakati akijibu swali Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Prof. Patrick Ndakindemi.

“Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara yenye kilomita 13 kuanzia Rau Madukani-Mamboleo- Shimbwe Juu katika Jimbo la Moshi Vijijini,” ameuliza Prof. Ndakindemi

Ahadi hiyo, ilitolewa na aliyekuwa Rais Hayati John Pombe Magufuli.

Akijibu swali hilo, Silinde amesema, Serikali imeendelea kutekeleza ahadi zilizotolewa na marais walizozitoa katika awamu zote kwa awamu.

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

“Mwaka wa fedha 2018/19 na 2019/20, Serikali imejenga kipande cha barabara chenye urefu wa mita 288 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi milioni 190 katika barabara ya Rau Madukani-Mamboleo-Shimbwe Juu,”amesema Silinde

“Mwaka wa fedha2018/19, barabara hii ilifanyiwa matengenezo ya muda maalum yenye urefu wa kilometa 9 kwa kiwango cha changarawe ambayo iligharimu Sh.148.85 milioni,” ameeleza.

Amesema, vilevile mwaka wa fedha 2021/22, barabara hii imetengewa bajeti ya Sh.10 milioni kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi yenye urefu wa kilometa 2.

“Serikali itaendelea na ujenzi na matengenezo ya barabara nchini ikiwemo Moshi Vijijini kwa kadri ya upatikanaji wa fedha,”amesema

Silinde amesema, Tamisemi iko katika mpango wa kuainisha ahadi zote za viongozi wakuu wan chi zilizitolewa, ili ziweze kutekelezwe.

error: Content is protected !!