April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ahofia ahadi ya Rais Magufuli kutotekelezwa

Spread the love

MBUNGE wa kuteuliwa, Alhaji Abdalah Bulembo (CCM) ameonesha wasiwasi kuwa, ahadi zilizotolewa zinaweza kushindwa kutekelezeka kutoka na muda kubaki mfupi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Alhaji ameonesha wasiwasi hiyo leo bungeni wakati akiuliza maswali ya nyongeza kuhusu ucheleweshaji wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeini 2015 kuhusu ujenzi wa daraja linalounganisha tarafa tatu za Luimbo, Suba na Nyancha.

Akiuliza swali la nyongeza leo tarehe 8 Aprili 2019, Bulembo amehoji, ni lini serikali itatekeleza ahadi iliyotolewa na rais kuhusu ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa, muda uliobaki katika kukamilisha ahadi hiyo ni mfupi

Aidha mbunge huyo alitaka kujua kama serikali ipo tayari kujenga daraja hilo katika bajeti ya mwaka 2019/20, ili wananchi wa tarafa hizo tatu zinazounganishwa na daraja hilo waweze kupata faraja na kuondokana na adha wanayopata hasa wakati wa mafuriko.

Awali katika swali la msingi la mbunge Rorya Lameck Auto(CCM) ambaye alitaka kujua ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ujenzi wa daraja linaloumganisha tarafa tatu

“Wakati wa ziara ya kampeini za uchaguzi Mheshimiwa Rais alihaidi kujenga daraja linalounganisha tarafa tatu za Luimbo,Suba na Nyancha na tayari halmashauri imeisha peleka makadirio wizarani.

“Je,ni lini  serikali itatoa itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo,” amehoji Bulembo.

Akijibu swali hilo Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais –TAMISEMI amesema, hawezi kujua kama barabara hiyo itajengwa kwa fedha zilizopo ndani ya bajeti ya mwaka 2019/2020.

Amesema, ni lazima ahadi zote za rais zitekelezwa na kuwa, muda uliobaki unatosha kuweza kutekeleza ahadi hizo.

Waitara amesema, Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (TARURA) umefanya tathimini ya gharama za ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 30 ambalo litaghalimu kiasi shilingi bilioni.1.15.

error: Content is protected !!