Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka wanaume wasitengwe fursa za kiuchumi
Habari za Siasa

Mbunge ataka wanaume wasitengwe fursa za kiuchumi

Spread the love

 

MBUNGE wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro (CCM), Priscus Tarimo, ameiomba Serikali iweke mipango ya kuwawezesha wanaume kiuchumi, kama inavyofanya kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Tarimo ametoa ombi hilo, leo Alhamisi tarehe 27 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

“Je, ni nini mpango wa Serikali kuwawezesha kina baba nao kiuchumi, baada ya mpango wa Halmashauri wa kuwawezesha akina mama, vijana na watu wenye ulemavu, kuwa na mafanikio makubwa?”

Aidha, Tarimo ameiomba Serikali ibadilishe sheria inayotafsiri ukomo wa umri wa vijana, kuwa miaka 35, ili umri huo uongezeke hadi kufikia miaka 45, kwa ajili ya kutanua wigo wa wanaume kupata mikopo hiyo.

“Kwa kuwa katika kundi la vijana wanaokopeshwa ni vijana wa kiume na wa kike na katika Katiba yetu inawatambua kuanzia miaka 18 hadi 35. Kwa kuwa wanaume wazalishaji mali ni kati ya miaka 36 mpaka 45,” amesema Tarimo na kuongeza:
“Kwa sababu ni suala la kisera, Serikali iko tayari kuongeza umri mpaka miaka 45 ili wanaume waweze kunufaika na mikopo hiyo?”

Akijibu maombi hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Dk. Festo Dugange, amesema Serikali haikuwaweka wanaume katika makundi hayo, yanayoruhusiwa kupata mikopo ya halmashauri, kwa kuwa wao ni rahisi kupata mikopo katika taasisi binafsi za fedha.

“Lengo la mikopo hii ni kusaidia makundi maalum katika jamii, ambayo hayawezi kupata mikopo katika benki za biashara na taasisi za fedha. Kwa sababu ya masharti magumu, ikiwemo dhamana na riba kubwa,” amesema Dk. Dugange.

Naibu Waziri huyo wa Tamisemi amesema “hivyo, Serikali ilitoa kipaumbele kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kwa kuwa wengi wao hawakopesheki katika benki na taasisi za fedha.”

Dk. Dugange amesema, kwa sasa Serikali haikusudii kuanzisha mpango wa kuwawezesha wanaume au kina baba.

Akizungumzia mikopo inayotolewa na halmashauri, Dk. Dugange amesema, Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, zimeendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Ambapo, mikopo hiyo hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 kifungu cha 37A, inayoelekeza kutenga asilimia 10 ya mapato yanayokusanywa na Halmashauri. Kwa ajili ya mikopo ya kwa wanawake (4%), vijana (4%) na watu wenye ulemavu (2%).

Akijibu ombi la kuongezwa kwa muda wa ujana, Dk. Dugange amesema Serikali inachukua wazo lake, kwa ajili ya kulifanyia kazi.

“Ni kweli Serikali imeweka utaratibu huu wa mikopo kwa vijana wa kiume na kwa maana ya tafsiri ya vijana, ni wale wenye umri wa miaka 18 hadi 35,” amesema Dk. Dugange na kuongeza:

Kwa maana ya tafsiri hii ya kisheria, Serikali bado haijaweka mpango wa kuonegeza umri, kwa sababu lengo la mikopo hii ni kwa vijana, kwa maana ya ya wenye umri chini ya miaka 35.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

error: Content is protected !!