June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ataka wakunga watengewe fedha

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete, akiwa amembeba mtoto mchanga wa Rehema Twaribu

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, (CCM), Diana Chilolo ameitaka Serikali kutenga fungu kwa ajili ya kuwawezesha wakunga wa jadi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akiuliza swali bungeni leo amesema fungu hilo litawawezesha wakunga hao kuendelea kuwasadia wanawake wenye matatizo kwenye mazingira mazuri na vifaa vya kisasa.

“Wakunga wa jadi wana uwezo sawa wa kutibu na kuwasaidia kinamama wenye matatizo ya uzazi au wagumba lakini hutoa huduma hizo katika mazingira magumu na vifaa duni,” amesema.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe amesema  ni kweli wakunga wa jadi ni kiungo katika utoaji wa huduma za ukunga na jadi tangu miaka mingi iliyopita.

“Pamoja na kwamba huduma hizi zimekuwa zikitolewa lakini sio kwa kiwango kinachostahili.

“Wizara yangu inashirikiana na wakunga wa jadi kama watu muhimu katika jamii katika kuwatambua wanawake wajawazito wenye vidokezo vya hatari na kuwashauri kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya,” amesema .

Amesema wizara imekamilisha mwongozo wa huduma ya mama na mtoto katika jamii na kwamba ana imani kwamba wakunga hao watashiriki kikamilifu kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaimarika.

error: Content is protected !!