Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka Serikali iweke ruzuku kutibu wagonjwa kisukari, tezi dume
Habari za Siasa

Mbunge ataka Serikali iweke ruzuku kutibu wagonjwa kisukari, tezi dume

Spread the love

KUTOKANA na ongezeko la wagonjwa wa kisukari na tezi dume, Serikali imetakiwa kuweka fedha za ruzuku zitakazosaidia kutibu wananchi wasiokuwa na uwezo ili kunusuru maisha yao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma, leo Jumanne, Mbunge wa Igalula (CCM), Venant Protas, amesema watu wengi wanaosumbuliwa na maradhi hayo ambao hawana uwezo, wamekuwa wakisumbuliwa wanapoomba misamaha ya matibabu bure

“Kumekuwa na changamoto sana ya watu wanaokwenda kupata misamaha hasa wa kaya maskini anapokwenda pale hawapewi misamaha bali wanaulizwa maswali na kuambiwa wakatafute fedha, hamuoni kama wizara mtoe miongozo mahususi ili wapewe msamaha?” amesema Protas na kuongeza:

“Magonjwa haya yamekuwa makubwa sana hasa kwa kaya maskini kama tumeweka ruzuku kwenye mbolea na umeme, hamuoni kwa magonjwa haya ili kuokoa maisha tukaweka ruzuku ili wananchi wetu tuweze kuokoa maisha yao.”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amesema Serikali itaweka nguvu kuhakikisha wasiokuwa na uwezo wanapata matibabu bure kulingana na miongozo inavyotaka.

Aidha, Dk. Mollel amesema Serikali hutumia kiasi cha Sh. 300 bilioni kutibu wagonjwa wa kisukari na Sh. 46.42 bilioni kwa wagonjwa wa tezi dume.

“Magonjwa haya mawili tu kufikia Sh bilioni 346.42 wakati bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka ni shilingi bilioni 200. Hivyo, ikitokea huduma ya matibabu kwa magonjwa haya mawili kutolewa bure itapelekea huduma nyingine katika nchi kusimama,” amesema Dk. Mollel na kuongeza:

“Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2022/2023 gharama ya msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wa Sukari na Saratani ya Tezi Dume ilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 70.4.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!