July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ashauri matumizi vigae kuezekea kupunguza gharama

Dk. Leornad Chamriho

Spread the love

 

MBUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Leornad Chamriho ameshauri matumizi ya bidhaa zinazotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo viage kuezeka badala ya bati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo amesema hay oleo Ijumaa tarehe 17 Juni 2022 bungeni jijini Dododma akichangia mjadala wa hoja ya bajeti kuu ya Serikali.

Chamriho amesema vifaa vya ujenzi vinavyotumia malighafi zinazotoka nje zimepanda bei na hivyo kushauri matumizi ya vifaa vinavyotumia malighafi kutoka ndani.

Ameshauri matumizi ya vigae kuekeza kwasababu utengenezaji wake unatumia malighafi ambazo zinapatikana kwa urahisi hapa nchini.

“Miaka ya nyuma Serikali ilikuwa inatumia vigae kuekeza majengo yake na ni kweli vimedumu kwa muda mrefu lakini pia tulikuwa na kiwanda cha vigae ambacho malighafi yake ni udongo ambao tunao wakutosha na tunaweza kutumia gesi yetu kwaajili ya kuchoma,” amesema Chamriho.

Amesema matumizi ya vitu vya ndani vitasaidia kupunguza mfumuko wa bei za vifaa vya ujenzi ambavyo bei zake zimepanda katika soko la dunia.

Sambamba na hilo ameshauri wakandarasi wa ndani kujengewa uwezo wa kutekeleza miradi mikubwa ili kupunguza gharama za miradi.

“Serikali ifanya juhudi za makusudi ili kuwezesha wandarasi wa ndani kutekeleza miradi mikubwa kwa kuwatengea miradi ambayo itawasaidia kupata uzoefu.

Ametoplea mfano wa miradi iliyopewa wazawa ikiwemo daraja la Mbutu , barabara ya Dumila-Kilosa, Urambo-Kaliua, Makutano-Sanzate “tukiwatumia tutapunguza gharama za miradi kwasababu ya bei kubwaya wakandarasi wa nje.”

“Napendekeza Waziri afanye juhudi za kurekebisha sheria ya manunuzi au kuwatengea miradi ya kuwaongezea uwezo.”

Alishauri pia ili kuwa na matumizi mazuri ya fedha ni vyema kutumia vifaa bora vitakavyoakisi matokeo ya kudumu.

Amesema vifaa bora vina gharama kubwa lakini vinadumu kwa muda mrefu na hivyo kutaka Ofisi ya CAG kujengewa uwezo wa kufanya tathmini ya gharama ya mradi katika uhai wake.

“Huko majumbani tunaona unawez akununua bomba la Sh 5000 lakini ukawa unalibadilisha kila mwezi lakini ukinunua bomba la 15,000 linadumu miaka 15 na ukipiga hesabu unaona bora ununue la bei kubwa lenye ubora,” amesema.

error: Content is protected !!