Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ashauri kesi kubwa za rushwa DPP arukwe
Habari za Siasa

Mbunge ashauri kesi kubwa za rushwa DPP arukwe

Daniel Nsanzugwako, Mbunge wa Kasulu Mjini
Spread the love

MBUNGE wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako ameishauri serikali kuiruhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), kuendesha mashauri makubwa ya rushwa pasipo kupitia Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Nsanzugwako ametoa hoja hiyo leo tarehe 15 Aprili 2019 bungeni jijini Dodoma, akidai kwamba Ofisi ya DPP inakwamisha baadhi ya kesi za ufisadi.

Sambamba na kutoa hoja hiyo, Nsanzugwako alihoji bungeni, idadi ya kesi ambazo zimezuiliwa na Ofisi ya DDP.

“Kwa nini TAKUKURU wasiachwe kuendesha mashauri makubwa ya ufisadi na wizi moja kwa moja bila ya kuomba kibali cha DPP? Swali B linauliza kesi ngapi DPP amezuia majalada hayo ya watuhumiwa?”

Nsanzugwako amedai kuwa “Halamshauri ya mji wa Kasulu tuliibiwa fedha takribani bil 5.9 inagawa baadae nasikia uhakiki ulibainisha takribani bil 2 ziliibiwa pale, watuhumiwa walisimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi, lakini cha ajabu watuhumiwa hao hawajafikishwa mahakamani eti DPP hajatoa kibali.”

Akijibu swali la Nsanzugwako, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dk. Marry Mwanjelwa amesema si kweli kwamba DPP anazuia majalada ya uchunguzi yasifikishwe mahakamani, na kwamba kuna baadhi ya majalada huchelewa kufikishwa mahakamani, huku mengine yakikosa nguvu ya kisheria katika kufunguliwa.

“Kwenye majibu yangu ya msingi nimesema DPP ni ofisi inayojitegemnea, kwa maana kwamba sio amezuia isipokuwa majalada haya yamechelewa, KasuLu sio kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa bilioni 5.9  Kasulu kulikuwa na ubadhirifu wa milioni 1.6.

 Na kulikuwa na kesi 12, kesi  6 zilifutwa sababu zilikosa ushahidi, na tano zimesua sua sababu ya mashahidi kuogopa kutoa vielelezo, watazania wawe na kiu ya kutoa ushirikiano kwa taasisi yetu ya kupambana na rushwa,” amesema Dk. Mwanjelwa.

Dk. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, Ofisi ya DPP inajitegemea na hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi, inayoipa mamlaka ya kufungua, kusimamia na kuendesha  mashtaka yote nchini.

“Dhana ya DPP anazuia majalada ya uchunguzi yasifikishwe mahakamani si sahihi, DPP ni ofisi inayojitegemea na majukumu yake yako kwa mujibu wa sheria, hata hivyo sote tumeshuhudia kwamba viongozi wa serikali ikiwemo mawaziri kufikishwa mahakamani kisha kupelekwa jela,” amejibu Mwanjelwa.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007,  Takukuru wanayo mamlaka ya kufikisha mtuhumiwa waliotenda makosa ya hongo kinyume na kifungu cha 15 sheria hiyo, moja kwa moja mahakamani bila kwa DPP,

 Makosa mengine yaliyosalia yanapaswa kupata kibali cha DPP yanapaswa kupata kibali cha  kama ilivyo elekezwa kwenye kifungu cha 51 1 cha sheria namba 11 2007, kwa mujibu wa kifungu cha 57 (2) cha sheria hiyo, DPP anapaswa kutoa au kutotoa kibali cha kuwafikisha mahakamni ndani ya siku 60 tangu jalada la uchunguzi kumfikia,”

Akikazia hoja hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi amesema “Mwanasheria mkuu wa serikali- mamlaka ya dpp kw amujibu w akatiba, ambayo inampa dpp uwezo wa kufungua kuendesha na kusiammaia mashtaka yote nchini.

Hazuii anatoa kibali au anatoa kibali, lakini hafanyi hivyo  anachofanya dpp kwa sababu yeye sio mamlaka ya uchunguzi bali ya mashataka lazima apime Kama anaokwamba ushahidi ulioletwa katika malaka ya uchunguzi hauwezi kufuangua mashtaka hatotoa kibali mpaka atakopojiridhisha ushahidi unajitosheleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!