January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ashangaa Prof. Ndulu, Waziri Mkuya kutowajibishwa

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya

Spread the love

MBUNGE wa Mpwapwa, Greogory Teu (CCM) ameshangazwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benu Ndulu kutowajibishwa kutokana na kuanguka kwa shilingi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Amesema, si jambo la kawaida kuona shilingi ya nchi ikiporomoka kwa kiwango kikubwa huku viongozi wa nchi wakiendelea kuwa salama.

Kutokana na hali hiyo amesema, ni lazima hatua zichukulie mapema ili kukabiliana na suala la kushuka kwa shilingi kwa sababu suala hilo ni kubwa.

Kutokana na kuporomoka kwa shilingi suala hilo linaenda pabaya hivyo ni lazima Waziri Saada na Prof. Ndulu wachukua hatua za haraka kuhakikisha  tatizo hilo linatafutiwa ufumbuzi wa haraka.

“Suala hili la kuporomoka kwa shilingi si jambo dogo kama linavyofikiriwa, kwani katika baadhi ya mataifa viongozi wangekuwa katika hali mbaya.

“Naomba Waziri wa Fedha na gavana wahakikishe wanatumia kila mbinu kumsaidia rais kuhusiana na kuporomoka kwa shilingi, suala hili ni kubwa nchini kwa sababu hali iliyofikia sasa inaenda kubaya, tatizo hilo ndio litaleta hali mbaya ya maisha kwani wakiacha dola itafikia sh. 3,000 jambo ambalo halifai,” amesisitiza Teu.

Pudensiana Kikwembe (Viti Maalumu-CCM) amesema, umefika kwa kizazi kilichopo watu kikubali kuingia gharama kwa ajili ya kizazi kijacho, ili kuhakikisha asilimia 50 hadi 70 watu waishio vijijini wanawekewa umeme, hivyo alishauri tozo ya mafuta iendelee.

Pia amesema, matumizi ya Mashine za Kielektroniki (EFD) yafanyiwe utaratibu na wananchi waelimishwejuu ya umuhimu wa kulipa kodi.

Dk. Kikwembe amesema, jambo ambalo linasababisha kulaumiwa ni kutokana na serikali kutokuwa na nidhamu ya bajeti.

Amesema,  jambo la kutokuwa na nidhamu ya bajeti kunasababisha matumizi makubwa zaidi ya kiwangokilicho pitishwa na bunge.

Pia ametaka Serikali kudhibiti wezi, wabadhirifu na ufisandi ndani ya taasisi za serikali ili fedha zilizotengwa ziweze kuwa na manufaa.

Akichangia katika mdajala huo Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Ester Matiku ameitaka serikali kuongeza wigo wa kodi kwa kuangalia nyumba pamoja na nyumba zenye milango ya maduka ya biashara ambayo wamiliki wamekuwa wakipata fedha nyingi  kutokana na malipo ya wapangaji ambazo zimekuwa hazilipwi kodi.

 Mbali na hilo amekema ubadhirifu wa katika miradi ya maendeleo na kutolea mfano mradi wa mabasi yaendayo kasi kuwa yanaubadhirifu mkubwa ambao amesema atahakikisha atauibua wakati wa bunge lijalo atakapokuwa amerejea bungeni.

error: Content is protected !!