June 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge alizwa milioni 4.8

Spread the love

WATU saba wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Tuhuma za kumwibia Sh 4.85 milion, Angel Kiziga Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa hao ni Richard Sivina (31), Richard Mlaki (26) Rashid Almando (36), Seleman Hussein (35), Omar Sadiq(30), Jamal Mohammed(25), na Juma Ndaigwa.

Akisoma Mshtaka hayo Hellen Mushi Wakili wa Serikali mbele ya Dk Yohona Yongola Hakimu Mkazi katika Mahakama hiyo amedai kuwa watu hao tarehe 1Juni mwaka huu katika Jiji la Der es Salaam walitenda kosa hilo la kuiba fedha hizo kutoka kwa Adam Hussein mali ya Angel Kiziga.

Watuhumiwa walikana mashtaka hayo na kupewa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini hati ya dhamana ya Sh 1 Milion kila mmoja.

Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 Julai mwaka huu.

error: Content is protected !!