Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari Mbunge alilia walimu wa kike shule Birise, Donsee
Habari

Mbunge alilia walimu wa kike shule Birise, Donsee

Spread the love

 

KUNTI Majala, Mbunge Viti Maalumu mkoani Dodoma, ameiomba serikali kupeleka walimu wa kike katika Shule za Msingi Birise na Donsee, zilizoko mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Majala ametoa ombi hilo leo Alhamisi tarehe 4 Februari 2021 bungeni jijini Dodoma, ambapo ameihoji Serikali lini itapelek walimu wa kike katika shule hizo ambazo hazina walimu hao.

Akijibuwa ombi hilo, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ameeleza kwamba serikali inatambua changamoto hiyo na kwamba inajiandaa kuweka mpango wa ajira na mgawanyo wa walimu wapya katika halmashauri zote nchini.

Aidha, TAMISEMI imeagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha inaweka idadi sawa ya walimu kwa kuzingatia jinsia.

“Wakati serikali ikijiandaa na mpango wa ajira na mgawanyo wa walimu wapya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI inazielekeza Halmashauri zote nchini kufanya msawazo wa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari,” ameagiza.

Hata hivyo, Waziri wa TAMISEMI amesema wizara yake imepeleka mwalimu mmoja wa kike katika Shule ya Msingi Donsee, wakati ikiendelea kukamilisha taratibu za kumpeleka mwalimu wa kike katika Shule ya Msingi Birise.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!