MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) nchini Tanzania, Fakharia Shomr Khamis ameitaka Serikali kueleza ni maslahi yapi askari polisi anayapata pindi anapopata madhira akiwa kazini ikiwemo kuuawa. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo…(endelea).
Fakharia amehoji hayo leo Alhamisi tarehe 9 Septemba 2021, bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu akisema kuna askari hupata ulemavu wakiwa kazini.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Chilo amesema, jeshi la polisi lina utaratibu na kanuni ya fadia kwa askari wanapopata tatizo wakiwa kazini.
“Ikitokea amepata shida katika harakari za kazi za kiasikari, kupitia kanuni hiyo ya polisi na magereza huwa wanapata fidia kwa kiwango kutokana na tatizo lenyewe kama kuumwa, ulemavu na kifo,” amesema Chilo
Katika swali la msingi, Fakharia aliuliza serikali inatoa kauli gani kuhusu usalama wa askari ambao wakati mwingine huvamiwa na kejeruhiwa na kuporwa silaha wakati wakiwa kazini.
Chilo akijibu swali hilo amesema, askari wa jeshi la polisi wapo imara katika kutumiza majukumu ya kazi zao za kila siku na wamepata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya mbinu za medani, matumizi ya silaha ya kujihami.
Pia katika utendaji kazi wao hufata utaratibu wa kujilinda na kulinda wengine, ila mazingira na maneno ya utendaji kazi husababisha changamoto mbalimbali kutokea kama hizo za kuvamiwa na kujeruhiwa.
Naibu waziri huyo amesema, mara zote jeshi la polisi hudhibiti hali hiyo na kushughulikia kwa haraka matukio ya namna hiyo na kuimarisha amani na utulivu.
Leave a comment