January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge alilia hospitali ya Tunduma, Serikali yamjibu

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM), Juliana Shonza ameitaka Serikali ieleze ni lini jingo la Hospitali ya Tunduma, Mkoa wa Songwe litafunguliwa. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Shonza ameihoji serikali bungeni jijini Dodoma leo Jumatano, tarehe 8 Septemba 2021 wakati wa kipindi cha maswalina majibu.

”Je, ni lini jengo jipya la Hospitali lililojengwa Tunduma litafunguliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi,” ameuliza Shonza.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi -Tamishemi, David Silinde amesema, Serikali inaendelea kutoa fedha za ukarabati na ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya ambapo imetenga Sh. 1.5 bilion kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo.

“Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga Sh.1.5 bilioni kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya Tunduma.” amesema Silinde

“Mradi huu ulianzwa kujengwa katika mwaka wa fedha 2016/2017, ambapo mpaka sasa Serikali imetoa Sh.14.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali nne katika Mkoa wa Songwe huku Halmashauri ya Mji wa Tunduma ikiwa ni mojawapo.

Aidha amesema kuanzia Julai 2021 jengo hilo lilianza kutumika kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje na kliniki ya mama wajawazito na watoto, ambapo ujenzi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza utahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) uliogharimu Sh.4 bilioni na upo katika hatua za umaliziaji.

Silinde ambaye ni mbunge wa Tunduma (CCM) amesema “Serikali imeendelea na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma ambao mpaka kukamilika inakadiriwa kugharimu Sh.9.5 bilioni.”

Akiuliza swali la nyongeza, Shonza ameuliza kwamba wananchi wa Tunduma wanataka kusiki kutoka kwa mbunge wao (Silinde), juu ya serikali hiyo itakamilika lini.

Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alionesha kufurahia swali hilo kwani ikizingatiwa mbunge anayepaswa kujibu ndiye anayeulizwa na kutaka waziri mwenyewe wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu kujibu.

Hata hivyo, Silinde alijibu akisema, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha Hospitali hiyo inakamilika.

error: Content is protected !!