January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge akumbushia ahadi ya Kikwete

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akmnadi Mgombea ubunge jimbo la Nkenge Bukoba Vijijini Assumpta Mshana

Spread the love

MBUNGE wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM) ameibana serikali bungeni na kutaka itoe kauli ya lini itatekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete katika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Omukajunguti. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mbunge huyo pia alihoji ni lini wananchi wa eneo hilo watalipwa fidia na kama fidia hiyo itazingatia viwango stahiki kulingana na soko la sasa.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charlesi Kitwanga alikiri kuwepo kwa ahadi hiyo na kwamba, serikali ina mpango wa kujenga kiwanja hicho.

“Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja kipya cha ndege katika Mkoa wa Kagera kitakachokuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa katika eneo la Omukajunguti lenye ukubwa ekari 2400,” amesema Kitwanga.

Alisema, eneo hilo linahusisha vitongoji vya Mushasha, Bulembo na Bugorora ambavyo ardhi yake itachukuliwa kwa kazi hiyo.

Amesema, uthamini wa mali za wakazi wa maeneo hayo umefanyika tangu mwaka 2010 na ulibaini kuwa jumla ya Sh. 12 bilioni zinahitajika kwa ajili ya kulipa fidia.

Naibu Waziri huyo amesema, serikali itaanza kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa kwa ajili ya kuendeleza Kiwanja cha Ndege cha Omukajunguti kuanzia mwaka wa fedha wa 2015/16.

Kwa mujibu wa Kitwanga, malipo ya fidia hiyo yataangalia thamani halisi ya fedha katika soko ambapo licha ya kuwa wamechelewa kulipa lakini hakutakuwa na malalamiko.

error: Content is protected !!