August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge akumbuka wanawake Sumbawanga

Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Aesh Hilaly

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Sumbawanga mjini, Aesh Hilaly (CCM), ameahidi kukabidhi vitanda vitano maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito pamoja na magodoro 10 kwa ajili ya  kituo cha afya cha Mazwi mjini Sumbawanga, anaandika Mwandishi Wetu. 

Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika kata ya Mazwi alisema kuwa atatoa vitandanda hivyo vyenye thamani ya Sh. 180,000 lengo likiwa ni kuboresha huduma katika kituo cha afya cha Mazwi ili wakina mama wajawazito waanze kujifungulia katika kituo hicho. 

Amesema wakinamama wa kata hiyo bado wanategemea hospitali ya mkoa ya Sumbawanga ambayo ndiyo hospitali ya rufaa kwa mkoa wa Rukwa kwa kuwa idara ya afya imeamua kuboresha kituo cha afya cha Mazwi.

Mbunge huyo amesema kata hiyo ina watu wengi ni vizuri kuboresha kituo cha afya kilichopo kata kata hiyo ili huduma mbalimbali zipatikane hapo, lengo likiwa ni kuwaondolea usumbufu wananchi wa kata hiyo.

Amesema kutokana na hali hiyo watendaji wa kituo hicho hawanabudi kujituma na kufanya kazi kwa weledi mkubwa na huruma kwa wagonjwa ili waone kuwa eneo hilo ni salama kwao na hivyo wapende kutumia kituo hicho.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kupata huduma katika kituo hicho kwani halmashauri imejipanga kukiboresha ili kiwe kinatoa huduma za kisasa na waache kukimbilia katika hospitali ya mkoa hali ambayo itapunguza mlundikano wa wagonjwa.

Awali kabla ya kuhutubia mkutano huo wananchi wa Kata hiyo walimueleza mbunge wao kero mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kuwa ni pamoja na kuzuiliwa kulima bustani kando ya mto Lwiche ambapo wamekuwa wakilima bustani kwa miaka mingi.

error: Content is protected !!