June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge akerwa na majibu ya serikali

Sehemu ya mawaziri wa CCM

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Clara Mwatuka (CUF) amedai kuwa, mawaziri wengi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa na tabia ya kutoa majibu yasiyoridhisha kutokana na kutojiandaa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

“Serikali imekuwa ikijibu kwa mazoea, kila kitu ni tuta…, tuta…, ni lini hayo matuta yataisha? Ni kwanini mmekuwa mkijibu majibu ya aina hiyo?” amehoji Mwatuka.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo alitaka kujua kwamba, kuna mikakati gani ya kuwawezesha wakulima wa karanga?

Awali katika swali la msingi, Mwatuka alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wakulima wa Wilaya ya Masasi ambao wanalima karanga wanatiwa moyo na kuendelea kulima zao hiyo.

Mbali na hilo, aliitaka serikali ieleze ni mikakati gani ya kuwatafutia soko la uhakika la kuuza karanga kwa lengo la kuinua kipato cha wakulima hao.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema, karanga ni mojawapo ya mazao ya mbegu ya mafuta yanayozalishwa hapa nchini ikiwemo Wilaya ya Masasi na Nanyumbu.

Amesema, uzalishaji wa karanga nchini umekuwa ukiongezeka kila mwaka hadi kufikia tani 1,835,933 mwaka 2014/15 kutoka tani 651,397 ya mwaka 2010/11.

error: Content is protected !!