July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge akataa taarifa ya Waziri kuhusu sakata la loliondo,

Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Spread the love

 

MBUNGE wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai, amekataa kupokea taarifa ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete, iliyoeleza kuwa Serikali haichukui ardhi ya Pori Tengefu la Loliondo, mkoani Arusha,. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akichangia bungeni jijini Dodoma, Oleshangai amedai kinachofanyika Loliondo ni unyakuaji wa ardhi kwani wananchi na Serikali ya vijiji husika hazijashirikishwa katika zoezi hilo kama sheria inavyoelekeza.

Awali, Ridhiwani alisema Serikali haichukui ardhi hiyo bali inaweka mawe kuonesha mipaka baina ya ardhi ya vijiji na ardhi inayotumika kwa ajili ya shughuli za hifadhi.

Fuatilia kiunganishi hiki kuona mjadala kati ya Oleshangai na Ridhiwani kuhusu sakata hilo.

error: Content is protected !!