Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge aitaka serikali inusuru mgodi wa Mwadui
Habari Mchanganyiko

Mbunge aitaka serikali inusuru mgodi wa Mwadui

Mgodi wa Mwadui Shinyanga
Spread the love

 

MBUNGE wa Kishapu mkoani Geita, Boniphace Butondo, ameiomba serikali ichukue hatua za haraka kuunusuru Mgodi wa Almasi wa Mwadui, uliositisha uzalishaji tangu Aprili 2021, kutokana na kushindwa kumudu gharama za uzalishaju. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Butondo ametoa ombi hilo leo Jumatatu tarehe 10 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesema changamoto ya Mgodi wa Mwadui kusimamisha uzalishaji imesababisha Halmashsuri ya Wilaya ya Kishapu kukosa mapato na zaidi ya wafanyakazi 1200 kukosa mishahara kwa muda.

“Serikali ifanye jitihada ili utaratibu wa kupata fedha ufanyike, liko tatizo kubwa halmshauri ya Wilaya Kishapu na kwa serikali yenyewe inakosa mapato. Lini serikwli itakwenda kusimamia mabenki ili zitoe fedha?.

“Wako watumishi 1,200 katika mgodi wa Mwadui tatizo kubwa mishahara yao kusimama muda mrefu, lini serikali itamaliza tatizo hili ili watumishi waondoke na aza hiyo?” amehoji.

Mbunge huyo ameiomba serikali iisaidie Kampuni ya Williamson Diamond Limited ipate fedha za mkopo kwa ajili ya kuanza uzalishaji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya amesema, wizara hiyo iko katika jitihada za kuisaidia kampuni hiyo ili ipate fedha za kujiendesha.

“Wizara inafanya kila inavyowezekana kuona mgodi unarejea kwenye uzalishaji natambua wizara itafanya kila inalowezekana. Tunapozungumza uzalishaji almasi Tanzania, tunazungumzia mgodi wa Mwadui na tunatambua aza za watumishi kutopata mishahara, Serikali italifanyia kazi suala hilo,” amsema Prof. Manya.

Naibu Waziri huyo wa madini amesema “Wizara itafanya kila inavyowezekana iwe kuendelea na kuongea na watoa huduma  turejee katika uzalishaji, tukianza matatizo yote ya watumishi kutolipwa na mapato  vitapatiwa masuluhusho. Wizara itafanya ushawishi kwa mabenki na watoa huduma kufanya kazi kwa kukopwa baadae tuzalishe.”

Boniphace Butondo, Mbunge wa Kishapu (CCM)

Amesema mgodi huo utaanza tena uzalishaji baada ya maombi yao ya mkopo kukubalika na benki za hapa nchini kwa ajili ya kugharamia shughuli zao za uzalishaji kwa kipindi cha miezi mitatu hadi kufikia awamu nyingine ya mauzo ya almasi.

“Hali ya bei ya almasi kwenye soko la dunia kwa sasa inatarajiwa kuwa bora zaidi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2020,” amesema Prof. Manya.

Prof. Manya amesema mgodi huo umeyumba kiuchumi kutokana na anguko la bei ya almasi katika masoko ya dunia.

“Mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na Kampuni ya Williamson Diamond Limited ulismamisha shughili za uzalishaji mwezi April 2020 kutokana na kushindwa kumudu gharama za uzalishaji kufuatia anguko la bei ya madini ya almasi katika masoko ya dunia.

Prof. Shukrani Manya, Naibu Waziri wa Madini

“Anguko la bei ya almasi katika soko la dunia lilisababishwa na athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona mwishoni mwa 2019,” amesema Prof. Manya na kuongeza:

“Athari ya kuanguka kwa bei ya almasi kulisababisha bei ya wastani ya almasi katika mauzo ya mgodi huo kwa mwezi Machi 2020 kuanguka hadi kufikia dola za Marekani 131.13 kwa karati. Bei ambayo haikidhi gharama za uzalishaji wa mgodi huo. Kwa mujibu wa makadirio ya mgodi huo wastani wa bei unapaswa kuwa angalau dola 208.00 kwa karati ili mgodi uweze kukidhi ghrama za uzalishaji.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!