Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mbunge aipongeza shule ya Brilliant kwa kutopandisha ada
ElimuHabari

Mbunge aipongeza shule ya Brilliant kwa kutopandisha ada

Mbunge wa Viti Maalum Dk. Thea Ntara akimkabidhi cheti cha kumaliza kidato cha nne mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Brilliant iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki ( PICHA: MPIGA PICHA WETU)
Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum, (CCM), Dk. Thea Ntara, ameipongeza shule ya Brilliant kwa kutopandisha ada kwa miaka mine mfululizo na amezitaka shule binafsi nchini kuiga tabia hiyo na kuacha tabia ya kupandisha ada kiholela kwani kufana hivyo kunaweza kuwanyima fursa watoto wengine wa kitanzania kupata elimu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 12 ya kidato cha nne ya shule ya Brilliant iliyoko Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

Alimpongeza Mkurugenzi wa shule hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya elimu hivyo kusaidia jitihada za serikali katika kuinua elimu.

“Nimeambiwa kwamba pamoja na kupanda kwa gharama za maisha lakini nyinyi kwa miaka minne mfululizo hamjapandisha ada hata kidogo nawapongeza sana lakini nataka shule zingine ziige mfano wa Brilliant kwasababu mnatoa huduma zaidi kuliko kuangalia biashara,” alisema

Wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Brilliant Aziza Hussein kulia na Joseph Tarimo waakielezea kuhusu fuvu la binadamu wakati wa mahafali ya 12 ya shule hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo Mbezi Kimara kwa Msuguri mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mbunge huyo alisema mbali na kusaidia serikali kuboresha kiwango cha elimu lakini uwekezaji huo mkubwa umesaidia pia kupunguza tatizo la ajira kwani amefanikiwa kuajiri wafanyakazi wengi kuanzia watumishi walimu, wapishi, walinzi madaktari na wauguzi.

“Kwenye risala nimesikia kwamba mlikuwa na mmefanya vizuri sana kwenye mitihani ya utahimilifu kwa kupata daraja la kwanza 49, daraja la pili 40 na watatu daraja la tatu sasa kwa matokeo haya ni imani yangu kwamba mtafanya vizuri sana kwenye mtihani wa mwisho mnaotarajia kuufanya hivi karibuni,” alisema

Mbunge huyo alimpongeza Ofisa Elimu Wilaya ya Ubungo na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwani usimamizi wao ndio umeiwezesha shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kitaaluma na kupanda madaraja kiwilaya, kimokoa na kitaifa.

Pia aliwakumbusha wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kulipa ada kwa wakati ili kuiwezesha shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwa kupata mahitaji muhimu.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza aliahidi kuwa shule hiyo itaendelea kutoa elimu bora kwa gharama nafuu ili kuwawezesha watanzania wengi kumudu kuwapeleka watoto wao shule.

“Ingawa gharama za maisha zimepanda zikiwemo gharama za uendeshaji lakini hatujapandisha ada kwa miaka minne mfululizo na tutaendelea kutopandisha ada ili watanzania wengi wamudu kupata elimu bora,” alisema Dk. Rweikiza

Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo, Edrick Philemon alisema kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 wanafunzi 13 walipata  daraja la kwanza, wanafunzi 26 daraja la pili na wanafunzi 27 daraja la tatu.

Alisema kwa mwaka 2021 wanafunzi 18 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 38 daraja la pili, wanafunzi 18 daraja la tatu ambayo ni mafanikio makubwa kwa shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

error: Content is protected !!