Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Mbunge aibua tuhuma nzito: “Serikali inawawekea vikwazo wananchi Ngorongoro”
Habari

Mbunge aibua tuhuma nzito: “Serikali inawawekea vikwazo wananchi Ngorongoro”

Spread the love

MBUNGE wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai ameituhumu Serikali “inawawekea vikwazo vya kimaendeleo” wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa kuhamisha fedha za miradi kwenda Handeni mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ole Shangai ameyasema hayo Bungeni leo Jumatato tarehe 13 Aprili 2022, wakati akichangia hoja ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake ya mwaka 2022/23.

Licha ya kumshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kukubali kusikiliza maoni ya wananchi na kuwataka kuhama kwa hiari Ole Shangai alidai kuna tatizo la wanaobaki kuwekewa vikwazo.

“Kuna tatizo moja, wale wanaobaki inaonekana Serikali wanawawekea vikwazo vya kimaendeleo, kuna fedha ambazo zilipelekwa kwaajili ya vituo vya afya, kwaajili ya maji, kwaajili ya madarasa inaonekana sasa Serikali inaamisha zile fedha kwenda Halmashauri ya Handeni. Walimu wameandikiwa, vituo vya afya vimeandikiwa hizo fedha ziende Handeni.

“Ninachojiuliza sasa Serikali imeona wa muhimu ni wale walio na hiari ya kuondoka na wale watakaobaki itakuwaje. Kama tunawanyima vituo vya afya, maji, shule je wale wananchi watakuwa sehemu ya Watanzania?” alihoji.

Baada ya kuibua tuhuma hizo Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa aliomba kumpa taarifa na kueleza bungeni hapo kuwa Serikali inapeleka miradi Handeni na Ngorongoro pia.

“Wananchi wote ni wakwetu kule Handeni tunapeleka maendelo lakini pia Ngorongoro miradi inaendelea, asubiri bajeti yangu aone namna tulivyojipanga kuahakikisha hata tarafa ya Ngorongoro inaenda kama kawaida,” amesema Bashungwa.

Hata hivyo Ole Shangai alikataa kupokea taarifa hiyo kwa kuhoji sababu ya wananchi wa tarafa hiyo kusubirishwa bajeti ijayo huku fedha walizokuwa wamepewa zikihamishwa kutoka kenye akaunti kwenda Handeni.

“Fedha Sh 500 milioni za kituo cha afya Nainokanoka zimehamishwa kupelekwa Handeni, Sh 600 milioni za maji kata za Ailelai, Masamburai, Olbalbai na maeneo mengine mnahamisha kwaajili ya kuwawekea wananchi vikwazo vya maendeleo,” amesema Ole Shangai.

Waziri wa Maji Juma Aweso naye aliomba kumpa taarifa Mbunge huyo na kueleza kuwa hakuna maelekezo yeyote ya Serikali kwamba wananchi wa Ngorongoro wasipelekewe maji.
“Katika jimbo la Ngorongoro tumepelaka mitambo ya kuchimba maji na Waziri Mkuu alielekeza wananchi wapate huduma ya maji katika jimbo hilo,” amesema Aweso.

Licha ya kuipokea taarifa hiyo Ole Sangai alidai kuwa maji hayo hayachimbwi tarafa ya Ngorongoro bali ni katika tarafa zingine za Loliondo na Sale.

Ameongeza kuwa hata Hospitali ya Enduleni iliyokuwa inapata Sh 500 milioni kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwaajili yakuwatibu watu, fedha hiyo imeondolewa pia.

“Kwahiyo watoto wa dogo, kina mama wanakufa kwa kukosa huduma, hasa serikali gani hii ambayo inawawekea vikwazo wananchi.

“Kama tunataka kupunguza wananchi Ngorongoro sio kwa namna hiyo ya kuwawekea vikwazo vya kimaendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Godwini Mollel naye alimpa taarifa kuwa Sh 321 milioni za Global Fund zimetengwa kuelekea eneo la Enduleni, “naomba mheshimiwa mbunge usiwe na hofu.”

Lichaya taarifa ya Naibu Waziri, mbunge huyo aliendelea kulalama kuwa vituo havina dawa na kwamba hata wananchihivi sasa wanakaguliwa kuingia getini na wanarudishwa.

Amesema suala lingine ni zoezi linaloendelea la Anwani ya makazi, “kule Ngorongo hakuna zoezi hilo katika tarafa ya Ngorongoro.”
Naye Naibu Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Methew amempa taarifa kuwa Serikali inajenga minara 24 katika Jimbo la Ngorongoro na zoezi la anwani za makazi linaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!