
Kimama wakinywa maji ya bomba
SERIKALI imetakiwa kueleza lini wananchi wataruhusiwa kunywa maji ya bomba moja kwa moja bila kuchemsha. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Maria Hewa (CCM), alihoji ni lini wananchi wataruhusiwa kunywa maji bila kuchemsha.
Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Maji, Amos Makalla amesema, maji safi na salama ni yale ambayo yanapita hatua zote za kusafisha na kutibu, hivyo huduma ya usambazaji wa maji mijini na vijijini inahusisha ujenzi wa miradi yenye miundo mbinu ya kusafisha na kutibu maji.
Hata hivyo amesema, ushauri wa kuchemsha maji ya kunywa ni tahadhari endapo uchafuzi utakaojitokeza kwenye mifumo ya usambazaji.
Amesema, serikali inaendelea na jitihada za upatikanaji wa maji safi na salama kwa kufanya maboresho ya mitambo ya maji na ujenzi wa miradi mipya mijini na vijijini.
More Stories
Kifo cha mtawa: Ni simulizi nzito
TAKUKURU: Rushwa ya ngono ipo, fichueni
Usiyoyajua kuhusu Panya wapima TB