May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ahoji ‘Kwanini tatizo la madawati haliishi?’ 

Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati darasani

Spread the love

UPUNGUFU wa madawati katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari nchini, umekuwa ni tatizo sugu. Je, serikali inachukua hatua gani endelevu za kuondoa tatizo hilo? Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ni swali la Boniface Mwita Getera, Mbunge wa Bunga alilolielekeza katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI- alilotaka kujua ma,ma serikali navyojipanga kumalizana na tatizo hilo.

Kutokana na swale hilo, TAMISEMI imeeleza kwamba, changamoto ya wanafunzi kukosa madawati katika Shule za Msingi na Sekondari imetokana na mwitikio mkubwa wa wazazi kuandikisha wanafunzi.

Na kwanza, idadi hiyo imeongezeka kutokana na kuanzishwa mpango wa utoaji wa elimu bila malipo ambapo idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kwenye hizo, umeongezeka maradufu.

“Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati ambapo madawati 5,070,896 yameongezeka na kufanya idadi ya madawati kuongezeka kutoka madawati 3,024,311 yaliyokuwepo mwaka 2015 hadi kufikia madawati 8,095,207 Septemba, 2020. 

“Katika kukabiliana na upungufu wa madawati, serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya utengenezaji wa madawati kwenye miradi yote inayotengewa fedha za ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa Shule za Msingi na Sekondari.

“Pia kuhamasisha wananchi na kuwashirikisha wadau na Asasi mbalimbali katika utengenezaji wa madawati pamoja na kuendelea kutenga fedha ya matengenezo ya madawati kwenye Halmashauri kupitia mapato ya ndani,” imeeleza wizara hiyo.

error: Content is protected !!