May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge adakwa akitazama video za ngono bungeni

Spread the love

CHAMA cha Conservative kutoka nchini Uingereza kimemsimamisha uanachama Mbunge wa Jimbo la Tiverton na Honiton, Neil Parish baada ya kubambwa akitazama video za ngono akiwa bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbunge huyo (65) kutoka chama cha Conservative amekumbwa na mkasa huo mzito baada ya wabunge wenzake wawili wa kike kutoa ushuhuda kuwa walimuona akitazama video hizo chafu kwa nyakati tofauti.

Jana tarehe 29 Aprili, 2022 wabunge hao wamesema walimuona Parish akiangalia video hizo chafu akiwa bungeni na kwa mara ya pili alikuwa katika vikao vya kamati.

Aidha, kutokana na kashfa hiyo mbunge huyo aliyedumu bungeni kwa zaidi ya miaka 12, amekiri kufungua ‘file’ la video hizo kwa bahati mbaya.

Pia amejitetea kwamba atakuwa tayari kutoa ushirikiano wote kwa wahusika wa uchunguzi wa sakata hilo.

Hata hivyo, mke wa mbunge huyo amemtetea mumewe na kudai kuwa ni mtu mwema na hajawahi kuwa na tabia hiyo katika kipindi cha miaka 40 ya ndoa yao.

Aidha, amesisitiza kuwa watu hawatakiwi kuangalia video za ngono kwani ni udharirishaji kwa wanawake.

Kutokana na mkasa huo, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wabunge wenzake wakimtaka Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson kumuwajibisha kwa kumuondoa madarakani.

Wabunge wengine hasa wa kike akiwemo Harriet Harman Kutoka chama cha Labour amemtaka ajiuzulu wadhifa wake kwani hafai kuwa mbunge na haoneshi picha nzuri kwa jamii.

Naye Waziri Rachel Maclean amepigilia msumari kuwa mbunge huyo anatakiwa kujiuzulu mara moja.

error: Content is protected !!