Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, wenzake wapinga kitabu cha mahabusu
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, wenzake wapinga kitabu cha mahabusu

Spread the love

 

MAWAKILI wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, wameweka pingamizi dhidi ya kitabu cha kumbumbuku za mahabusu, chenye taarifa zinazoonesha mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling’wenywa aliwekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Kati cha Dar es Salaam. Anaripoti Rehina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Pingamizi hilo limewekwa leo Jumatano tarehe 10 Novemba 2021, mahakamani hapo mbele ya Jaji Joackim Tiganga, baada ya SP Jumanne Malangahe, shahidi wa kwanza wa jamhuri katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya Ling’wenya, yasipokelewe kama ushahidi wa upande wa mashtaka, kuomba kipokelewe kwa ajili ya utambuzi.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alipinga kitabu hicho akidai wakati akitoa ushahidi wake mahakamani hapo, shahidi huyo hakuweka msingi wa upokelewaji kitabu hicho pamoja na kuthibitisha kupitia mlolongo wa taarifa za vizuizi vya mahabusu, kuwa ni cha Kituo cha Polisi cha Kati cha Dar es Salaam.

Wakili Mtobesya alidai shahidi huyo ambaye ni Mkuu wa Upelelzi Wilaya ya Arumeru Mkosni Arusha, alipaswa kujenga msingi kuonesha kuwa ni cha kituo hicho, huku akitaja hoja nyingine kuwa ni ili kitabu hicho kipokelewe kwa ajili ya utambuzi kinatakiwa kikidhi vigezo vya kisheria.

Aidha, Wakili Mtobesya alida kuwa, wakati akitoa ushahidi wake, SP Jumanne hakuieleza mahakama hiyo lini alikiona kitabu hicho, baada ya kukiona tarehe 7 Agosti 2020 kituoni hapo.

Naye Wakili Peter Kibatala amedai shahidi huyo hakuhojiwa na mawakili wa jamhuri kuhusu nyaraka hiyo kwa kuwa haikuileta yeye bali ililetwa na aliyekuwa shahidi wa upande wa mashtaka Ricado Msemwa, katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adam Kasekwa yasipokelewe mahakamani hapo kwa madai yalikuwa kinyume cha sheria.

Kibatala amedai, wenzetu walitakiwa kuandika barua au hatua zingine nyaraka hii iwarudie mikononi mwao kwa sababu Mahakama na wao ni taasisi mbili tofauti.

Amedai, wamezua wasiwasi kama walivyoiomba na kumpatia shahidi hapa Mahakamani. Shahidi hakuongozwa kwa namna yoyote ile kuhusianisha kuwepo kwa nyaraka hii Mahakamani na yeye kuja kufanyia utambuzi.

“Nyaraka ilikabidhiwa na mtu mwingine kabisa. Hajazungumza chochote kati yake na shahidi Msemwa. Angekuwa yeye tungefumba macho kisheria. Kwa hili hajaonyesha uhusiano wowote kati yao,” amedai
Kitabu hicho kinaonesha, Lingwenya alipokelewa kituoni hapo tarehe 7 Agosti 2020, akitokea katika Kituo cha Polisi cha Kati Koshi mkoani Kilimanjaro alikokamatwa tarehe 5 Agosti mwaka jana kwa kosa la kula njama za kufanya vitenso vya kigaidi.

Katika keai hiyo, mawakili wa utetezi wanadai kuwa Ling’wenya hakuwahi fikishwa na au kuhojiwa kituoni hapo.

Baada ya mapingamzii hayo, mawakili wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando waliomba ahirisho kwa muda ili wajipange kuzijibu.

Jaji Tiganga alikubali ombi hilo na kuiarisha kesi hiyo kwa muda wa nusu na sasa kesi hiyo inaendelea kwa mawakili wa serikali kujibu hoja hizo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!