August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Viongozi Chadema kufungwa ni mkakati wa Serikali

Dk. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (Picha kubwa) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa kufungwa kwa baadhi ya viongozi wao akiwemo Diwani na Mbunge ni sehemu ya mkakati uliosukwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kudhoofisha nguvu ya upinzani, anaandika Moses Mseti.

Kauli ya Mbowe inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Suleiman Mathew Mwenyekiti wa Chadema mkoani Lindi, kuhukumiwa kifungo cha miezi nane gerezani kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara.

Itakumbukwa pia, tarehe 11 Januari mwaka huu Peter Lijuakali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero alihukumiwa kwenda gerezani kwa miezi sita kwa kosa la kufanya vurugu katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya Kilombero uliofanyikwa mwaka 2016.

“Tunalaani vikali viongozi wetu kukamatwa na kuhukumiwa gerezani, hatujwahi kusikia wala kuona viongozi wa CCM wakiwemo wabunge wakikamatwa na kuhumiwa gerezani lakini sisi kila kukicha tunakatamwa na kufungwa,” amesema Mbowe.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, viongozi wanaohukumiwa kwenda jela akiwamo mwenyekiti wa Chadema Lindi, wana haki kikatiba kufanya mkutano wa hadhara na kwamba anashangazwaa na uamuzi wa Mahakama.

Mbowe alikuwa akizungumza baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema ambapo pia walitangaza kumpokea rasmi na kumkabidhi kadi David Kafulila, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini.

Akitoa neno la shukrani Kafulila alisema, Chadema ni nyumbani kwake kwani chama hicho ndicho kilichomlea na kumtangaza katika uwanja wa kisiasa.

“Ukiwa kwenye treni au gari huwezi kuangalia mwendo isipokuwa ukiwa nje. Ndivyo hivyohivyo na sisi tuliokuwa nje ya Chadema tulikuwa tunaona mwendo wake kuwa ni mkali na unafaa,” amesema Kafulila.

Kafulila amesema kuwa, ameamua kurudi Chadema kwa sababu chama hicho ni chama cha mapambano na ni chama cha makamanda wanaopambana kutafuta haki, kama ilivyo kwake analivyopambana akiwa mbungeni 2010-2015.

error: Content is protected !!