April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Tumefika ukomo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kwa kuwa serikali imeweka pamba masikioni, nao wamefika ukomo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Hivyo, ameagiza viongozi wa chama hicho kuanza kufanya mikutano ya hadhara ya kudai Tume Huru, tarehe 4 Aprili 2020 bila kujali katazo la Rais John Magufuli.

Mbowe ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Machi 2020, wakati akizungumza na wanahabari kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Kwa kuwa wameweka pamba masikioni, na sisi tumefika ukomo wa kubembeleza. Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha.

“Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge.  Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie,” amesema.

Amesema, viongozi hao wanapaswa kufanya mikutano hiyo kwa mujibu wa sheria ya nchi (Katiba), hata kama mamlaka husika zitakataza.

https://youtu.be/EMsbeXXaHwU

“Tarehe 4 Aprili hatutasubiri kibali, tutaanza mikutano nchi nzima. Kwa kauli hii nawatangazia viongozi wote wa Chadema, viongozi wa kanda, mkoa, wilaya, kata vijiji na misingi.

“Tuanze kufanya mikutano ya hadhara kwa utaratibu ulioko kisheria, kudai vitu viwili. Tume Huru ya uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi wa urais na ubunge,” amesema Mbowe.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Kilimanjaro amesema, agizo hilo amelitoa baada ya jitihada za chama hicho kutaka meza ya majadiliano na Rais Magufuli, kuhusu suala hilo kugonga mwamba.

“Tumezungumza mara nyingi ulazima wa kuwa na Tume Huru, kwani ni uwendawazimu kwenda kwenye uchaguzi kwa mfumo huu na tume hii tukategemea uchaguzi wa haki. Hakika tunaipeleka nchi kwenye machafuko yasiyokua na sababu,” amesema Mbowe na kuongeza:

Amesema, viongozi wa Chadema walitumia Maadhimisho ya Siku ya Uhuru yaliyofanyika jijini Mwanza, mwishoni mwa mwaka jana pamoja na kumwandikia barua Rais Magufuli, kuomba maridhiano, lakini ombi lao halijafanyiwa kazi hadi sasa.

error: Content is protected !!