January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Serikali iwajibike mauaji ya albino

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman, ameitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwasaka na kuwakamata wauaji wa walemavu wa ngozi (albino) na vikongwe. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa Mbowe, Serikali ya CCM imeshindwa kuwalinda watu na mali zao wakiwemo albino ambao wanatekwa, kupotezwa na kisha miili yao kuokotwa ikiwa imekatwa baadhi ya viungo.

Amesema kuwa serikali imeshindwa kutumia intelijensia ya vyombo vyake kuwanasa wauaji wa albino kama itambavyo kupata taarifa za kiintelejesia za maandamano na mikutano ya wapinzani kuwa na vurugu na hivyo kuifutilia mbali.

Mbowe ametoa rai hiyo akiwa katika ziara ya kuimarisha chama Kanda ya Ziwa Magaribi, inayojumisha mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza.

Amesema mauaji hayo hayalitii aibu taifa pekee bali pia na watu wake kuonekana ni wanyama wasiokuwa na chembe ya huruma na wanadamu wenzao.

“Pamoja na mauji haya kushamili nchini, bado serikali ya CCM imekaa kimya na viongozi wakuu wa nchi akiwemo Waziri Mkuu Mizengwe Pinda, wameshindwa kuchukua hatua yeyote.

“Machozi ya Pinda yapo wapi, wakati ule mauaji haya yanatokea alitoa chozi lakini leo mauaji yanafanyika yupo kimya na hatua ameshindwa kuchukua,”anasema Mbowe.

Anaongeza kuwa; “vikongwe wanauawa kila kukicha kwa imani za kishirikina na mambo ya namna hii hayapaswi kuonekana, yanajenga taswira mbaya katika taifa letu”.

Kwa mujibu wa Mbowe, mauaji ya vikongwe sasa imefika miaka 20 tangu yaanze nchini huku yale ya albino yakitimiza miaka tisa lakini viongozi wameshindwa kuyadhibiti.

error: Content is protected !!