Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Segerea kuna mambo ya kuumiza
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Segerea kuna mambo ya kuumiza

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa amesema, amekutana na mambo ya kuumiza alipkuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Mbowe ambaye amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi mitatu amesema, ndani ya gereza la Segerea kuna ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja, kukosekana kwa mahitaji muhimu na msongamano wa watu kuliko uwezo wa magereza.

Mbowe abaye alisota rumande tangu mwezi Novemba 2018 kwa kukataliwa dhamana, aliachwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tarehe 7 Machi 2019.

Ni baada ya kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kukiuka masharti aliyopewa katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 15 Machi 2019 jijini Dar es Salaam, Mbowe ametaja changamoto zinazowakabili wafungwa katika gereza la Segerea huku akikazia kuhusu tatizo la wanaofungwa bila hatia.

Mbowe ameeleza kuwa, gerezani humo kuna changamoto ya mrundikano wa mahabusu uliosababisha mahabusu kuambukizana magonjwa ikiwemo ya ngozi unaofahamika kwa jina la burudani.

”Segerea kuna mahabusu kati ya 2300 mpaka 2450 lakini uwezo wa gereza hilo ni mahabusu 750, watu wanalala kitu kianaitwa ‘mchongoma’ yaani mnalala kwa ubavu mmoja kwa masaa matatu kisha mnageuka,” amesema Mbowe.

Mbowe ameshauri vyombo vya kutoa haki viweke mikakati ya namna ya kupunguza mahabusu, akidai kwamba vyombo hivyo kama vitapitia vizuri makosa ya mahabusu hao, itagundua kuwa nusu ya wafungwa walioko magerezani hawakustahili kuwepo huko.

”Sisi hatuna tatizo na mifumo yetu ya utoaji haki kwa maana ya mahakama lakini mahabusu wanavyoishi kule magerezani ni kama tayari wote wamehukumiwa na sio watuhumiwa,” amesema na kuongeza;

 ”Mimi niombe vyombo vyetu vya kulinda na kutoa haki kwa watu vitafakari namna ya kupunguza hawa mahabusu na kama wataamua kupitia vizuri makosa ya watu, watagundua nusu ya mahabusu wanaojaza magereza zetu ni watu ambao hawakustahili kuwepo kule.”

Aidha, Mbowe amedai kuwa, askari magereza wanakabiliwa na ukosefu wa sare huku akisema baadhi yao wanajinunulia sare.

”Askari magereza hawapewi sare bali wanajinunulia kwahiyo ukikuta mjanja mjanja anavaa vizuri ila ukikutana na aliyechoka kachoka kweli kweli, niombe tu wawezeshwe, kazi wanayoifanya kukaa na mahabusu sio ndogo kama tunavyodhani,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!