Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Nguvu ya umma imenitoa gerezani
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Nguvu ya umma imenitoa gerezani

Spread the love

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe amesema, kilichomfanya akafutiwa mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili ni “nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana nguvu yao ya dola.” Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mbowe amesema hayo jana Jumamosi, tarehe 5 Machi 2022 akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, alipokwenda kutembelewa na kupelekewa zawadi wa wanachama wa Chadema ikiwa ni siku moja kupita tangu aachiwe huru.

Mbowe na wenzake watatu ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliachiwa huru Ijumaa ya tarehe 4 Machi 2022, baada ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo ya ugaidi iliyokuwa imefikia hatua ya washtakiwa kujitetea.

Kutokana na uamuzi huo wa DPP, Jaji Joachim Tiganga aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, aliifuta na kuagiza watuhumiwa wote wanne Mbowe, Halfan Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya kuachiwa siku hiyohiyo agizo lililotekelezwa.

Akizungumza na wanachama hao, Mbowe alisema, nguvu ya Chadema ni umoja na upendo kwani hawana majeshi wala silaha “lakini umoja wetu umekuwa silaha yetu kubwa sana.”

“Silaha hii ya umoja ndiyo imenitoa mimi gerezani, sikutoka gerezani kwa sababu kuna mtu ananipenda, nimetolewa gerezani kwa sababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana nguvu yao ya dola ndiyo sababu nimetoka,” alisema Mbowe aliyekaa mahabusu siku 226.

Alisema, katika kipindi chote akiwa gerezani, alitembelewa na watu wengi wakiwemo wanachama wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali, “hadi watu wa magereza wakawa wanashangaa huyu mtu ni nani, wewe Mbowe una nini na hawa watu au unawatumia nauli waje.

“Watu wanakuja, basi linatoka Kyela, basi linatoka Kigoma, Mwanza, Simiyu, Njombe, Moshi, Arusha na kila mahali, sasa wote ule ni upendo na nimeoneshwa upendo wa hali ya juu na hili kwangu na familia yangu ni deni kubwa tunashukuru,” alisema.

Kuhusu mgogoro wa viongozi mkoani Mbeya, Mbowe aliugusia kidogo akisema “nimesikia yaliyotokea Mbeya, japo sijapata taarifa rasmi za kiofisi, sisi ni familia na wanapokosea wenzetu tuna wajibu wa kurekebisha na tunahitaji kuijenga familia ya Chadema kwa uaminifu mkubwa kila mmoja ana thamani kubwa katika chama hiki.”

“Tulianza kama chama kidogo lakini dunia inatutambua na hata CCM waliokuwa hawatutambui wametambua kupitia kesi hii, wametambua Chadema ni jeshi kubwa na hilo jeshi kubwa limekuwapo kwa sababu kuna mmoja, wawili, watatu na wannne,” alisema.

Alisema, pamoja na matatizo na hofu zilizopo “tuwe wazito sana kuwapoteza wenzetu, isiwe ndiyo utamaduni wetu, lazima tukumbatiane kama watoto wa mama mmoja na nguvu ya Chadema ni umoja na upendo wetu, hatuna majeshi hatuna silaha lakini umoja wetu imekuwa silaha yetu kubwa ssana.”

“Silaha hii ya umoja ndiyo imenitoa mimi gerezani, sikutoka gerezani kwa sababu kuna mtu ananipenda, nimetolewa gerezani kwa sababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana nguvu yao ya dola ndiyo sababu nimetoka,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

error: Content is protected !!