Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Najivika mabomu kumpongeza Samia “angeendeleza kiburi cha mtangulizi wake”
Habari za Siasa

Mbowe: Najivika mabomu kumpongeza Samia “angeendeleza kiburi cha mtangulizi wake”

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anatambua kuwa ni vigumu kuwaeleza Watanzania na dunia kwamba anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali maridhiano ya kitaifa ila anajivika mabomu kufanya hivyo kutokana na hatua njema iliyofikiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Amesema angeweza kuendeleza kiburi cha mtangulizi wake lakini kutokana na ushawishi wake na wanachadema na viongozi wa CCM wenye busara wamefikia pazuri.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara.

Amesema hakuna nchi duniani ambayo imeshawahi kujengwa kwa demokrasia dhoofu kwani demokrasia ikikua na uchumi utakua.

Aidha, amemuomba Rais Samia asikwazike pale ambapo Chadema watampinga kwa nguvu zote katika baadhi ya ajenda.

“Nchi yetu inahitaji Katiba bora, usidanganywe na yeyote kuondoka bila katiba bora, lazima kuwepo na katiba bora ili tusirudi tena kwenye zile chaguzi za kihuni… za watu wanaiba uchaguzi na kuwa huru mitaani.

“Yeyote anayeiba lazima awajibishwe, pale ambapo tunaamini sheria zitasimama kwenye haki wanaostahili, hazitamkandamiza yeyote ili kwa pamoja tulijenge Taifa salama, linaloitengeneza kesho ya watoto wetu kuwa kesho bora zaidi.

“Tutaendelea kuzungumza na ushirikiano lakini tukiwa makini kuliko makini yenyewe.Tutapiga jaramba mpaka kieleweke!” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!