
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na viongozi wengine wakiwasili mahakamani
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka yanayowakabiri. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Viongozi hao walioripoti Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam kama walivyotakiwa mapema leo, lakini walipofika waliondolewa dhamana na kuwekwa mahabusu.
Mchana huu viongozi hao akiwemo Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Salum Mwalim, Msigwa, Mnyika na Esther Matiko wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu mchana huu baada ya kutolewa Kituo Kikuu cha Polisi walipokuwa wameshikiliwa.
MwanaHALISI Online itaendelea kuwajulisha kinachoendelea mahakamani hapo
More Stories
Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani
Rais Mwinyi amwapisha mrithi wa Maalim Seif
Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya