Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe na wenzake mahakamani tena kesho
Habari za Siasa

Mbowe na wenzake mahakamani tena kesho

Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

VIONGOZI tisa wa Chama cha Demokrasia na Maanedeleo (Chadema), wanatarajiwa kutinga mahakamani tena kesho kusikiliza kesi inayowakabili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wanaotarajiwa kufika mahakamani kesho, ni pamoja na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa taifa wa chama hicho; Dk. Vicenti Mashinji, katibu mkuu; John Mnyika, naibu katibu mkuu na Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake taifa (BAWACHA).

Wengine, ni Salum Mwalimu, naibu katibu mkuu Zanzibar; Esther Matiko, mbunge wa Tarime Mjini; Mchungaji Peter Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini; Ester Bulaya na John Heche, mbunge wa Tarime Vijijini.

Viongozi hao wandamizi wa chama hicho ambacho ni kikuu cha upinzani nchini, wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali na uchochezi.

Mbele ya Hakim Mkuu Mkazi Mashauri, watuhumiwa wote wanadaiwa kutenda tendo hilo, tarehe 26 Februari mwaka huu.

Wamekana madai hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!