Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe mfungwa Na. 305, apigwa ‘para’
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe mfungwa Na. 305, apigwa ‘para’

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, tayari amevishwa gwanda na kuwa mfungwa rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake wengine wanne, bado wako katika gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, wanakotumikia kifungo cha miezi mitano, wakati wakisubiri kulipiwa faini ya mamilioni ya shilingi, kufuatia kupatikana na hatia kwenye makossa 12 kati ya 13 walioshitakiwa mahakamani.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mmoja wa wafungwa waliofungwa pamoja na Mbowe na ambaye tayari yuko uraiani, Dk. Vincenti Mashinji amesema, “nawashukuru sana walionisaidia kutoka gerezani, kwa kuwa maisha ya kule siyo ya kawaida.”

Dk. Mashinji alikuwa katibu mkuu wa Chadema kwa miaka minne mfululizo. Alikihama chama hicho wiki mbili zilizopita na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ameteka gerezani kutokana na michango iliyokusanywa na chama chake hicho kipya.

“Tulipofika gerezani, tulikabidhiwa magwanda za wafungwa (za rangi ya chungwa) na kunyolewa nywele zetu zote na kuwa kipara. Jana tulikuwa tunapangiwa genge (kundi) la kufanyika kazi,” ameeleza Dk. Mashinji.

Anasema, “mimi wakati jana nikiitwa, ili niwe huru, nilikuwa ndio napangiwa genge langu. Nilikuwa nimepelekwa hospitali. Mwenyekiti Mbowe na wenzetu wengine, niliacha wakisajiliwa ili nao wapangiwe magenge yao.”

“Nimeishi gerezani kwa siku moja. Lakini usiombe. Kule siyo mahali ambako mtu unaweza kujivunia ukamanda,” anasimulia Dk. Mashinji na kuongeza, “mimi nilipewa Na. 302.”

Anasema, Mbowe amepewa Na. 305, huku John Mnyika, mbunge wa Kibamba na Katibu Mkuu wa sasa wa Chadema, akipewa Na. 300. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, amekuwa mfungwa mwenye Namba 301.

Akisimulia zaidi, Dk. Mashinji anasema, “baada ya kufikishwa katika gereza hilo, tarehe 10 Machi 2020, majira ya jioni, jambo la kwanza lilikuwa kukabidhiwa kwa Mnyapara.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana alipokwenda Segerea kumtoa Dk. Mashinji, alimkuta na upara licha ya kufikishwa kwenye gereza hilo akiwa na nywele.

Mbowe na viongozi wenzake wa chama hicho, walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miezi mitano au kulipa faini ya jumla ya Sh. 355 milioni.

Kwenye kesi hiyo namba 112/2018, katika mashitaka 13 yaliyokuwa yakiwakabili, walikutwa kutenda kosa katika mashitaka 12 ikiwa ni pamoja na kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kati ya Februari 1 na 16, 2018.

Hata hivyo, Mbowe na wenzake walipelekwa katika gereza hilo kutokana na kushindwa kutimiza mashatri ya faini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!