Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Matiko wafutiwa dhamana
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Matiko wafutiwa dhamana

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewafutia dhamana, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mbunge wa chama hicho katika jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe na Matiko wamefutiwa dhamana kufuatia mahakama hiyo, kujiridhisha kuwa wanakwenda kinyume na masharti ya dhamana waliyopewa. 

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 23 Novemba na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema ameridhika kuwa washitakiwa hao wawili, wamekuwa na tabia ya kukiuka masharti ya dhamana.

Mara baada ya kusoma uamuzi huo, wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala, ametoa taarifa kwa kuieleza mahakama wataukatia rufaa uamuzi huo.
Tarehe 12 Novemba, mwaka huu, upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya kufutwa kwa dhamana kwa Mbowe na Matiko kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana.

Upande huo ulidai kuwa watuhumiwa hao walisafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kutoripoti kwenye kituo cha Mkoa wa Ilala.

Mawakili wa Serikali waliwasilisha ombi hilo kwa kile walichidai mwenendo dhaifu wa kuhudhuria mahakamani ilhali kesi hiyo ilikuwa hatua ya kusomewa maelezo ya awali.

Tarehe 1 Mbowe hakuhudhuria makamani hapo ambapo kesi yao ililikuwa ikisikilizwa, Matiko na Mbowe hawakuhudhuria mahakamani wakati kesi yao imepangiwa usikilizwaji wa awali.

Wakati Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Kibatala wakipambana kukata rufaa kwa ajili ya dhamana ya viongozi hao.
Jeshi la Polisi limewashikilia na kuwapeleka mahabusu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

Habari za Siasa

Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje

Spread the love  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika...

error: Content is protected !!