Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Matiko ‘ngoma bado mbichi’
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Matiko ‘ngoma bado mbichi’

Ester Matiko (wa mbele) na Freeman Mbowe (wenye fulana nyekundu) wakiwa chini ulinzi wakirudishwa rumande baada kusikilizwa rufaa yao katika Mahakama ya Rufaa
Spread the love

MAHAKAMA ya Rufani leo tarehe 18 Februari 2019 imeanza kusikiliza rufaa ya serikali ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kusikiliza rufaa ya dhamana ya Freeman Mbowe na Esther Matiko. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa na Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) leo wamefikishwa mahakamani hapo ili kuanza kusikilizwa kwa rufaa ya serikali.

Rufaa hiyo iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imelenga kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa tarehe 30 Novemba mwaka jana, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.

Upande serikali leo mbele ya jopo la majaji watatu ambao ni Gerald Ndika, Stella Mgasha na Mwanaisha Kwaliko uliwsilisha hoja mbili za kuomba rufaa namba 344 ya Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika iondolewe mahakani.

Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu akisaidiwa na Paul Kadushi amewasilisha hoja hizo ambapo ameiomba mahakama kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa, haina miguu ya kisheria na kwamba, ni kinyeme cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Nchimbi amedai kuwa, Jaji Rumanyika alipotoka kisheria kwa kuipanga na kuiita kwa ajili ya usikilizwaji huku akijua rufaa hiyo iliwasilishwa kinyume na kifungu cha 362 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo 2002.

Amedai kuwa, Jaji Rumanyika hakuwapatia muda na haki ya kutosha wa kuuzikiliza upande wao.

Peter Kibatala, wakili wa upande wa utetezi akijibu hoja za mawakili wa serikali amedai, Mahakama Kuu haikusikiliza rufaa iliyokuwepo mahakamani zaidi ya kusikiliza pingamizi ziliyowasilishwa na upande huo.

Kibatala amedai kuwa, rufaa hiyo haina mashiko na kuiomba mahakama hiyo kuitupilia mbali.

Jaji Mgasha kwa niaba ya jopo la majaji wenzake amesema, watazingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili na kwamba, watatoa uamuzi katika tarehe itakayopangwa.

Mbowe na Mtiko walifutiwa dhama yao tarehe 23 Novemba mwaka jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kueleza kuwa, walikwenda kinyume na masharti ya dhamana kwenye kesi ya  msingi ya uchochezi inayowakibili.

Katika kesi ya msingi, Mbowe Matiko na wengine saba wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

Wengine ni Mbunge wa Peter Msigwa, Iringa mjini; John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji.

Pia wamo Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda; Mbunge wa Kawe, Halima Mdee; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!