Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Matiko mahakamani tena
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Matiko mahakamani tena

Freeman Mbowe na Ester Matiko wakipelekwa gerezani
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, kesho Alhamisi, tarehe 30 Januari, wanarudi tena kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, “kuonana na hakimu” anayesikiliza kesi yao. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro na Matiko, wameshatimiza miezi miwili na siku saba gerezani, kufuatia uamuazi wa aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, kuamua kuwafutia dhamana.

Kwa sasa, Mashauri ni Jaji wa Mahakama Kuu. Ameteuliwa na Rais John Pombe Magufuli, Jumatatu iliyopita na tayari ameapishwa kufanya kazi hiyo.

Haijaweza kufahamika mara moja, iwapo Jaji Mashauri ataendelea kusikiliza shauri hilo ama atakabidhiwa kesi hiyo hakimu mwengine.

Kufuatia maamuzi hayo, Mbowe na Matiko, waliamua kukata rufaa mahakama kuu, kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu na kurejea uraiani. Kesi hiyo haijasilikizwa mpaka sasa, baada ya Jamhuri kuwasilisha rufaa mahakama kuu, kupinga kufutwa kwa mapingamizi yao waliyowasilisha mahakamani.

Wanasiasa hao wawili na wengine saba, wakiwamo wabunge watano wa Chadema, wanakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani yenye mashitaka 13 ya jinai yakiwamo uchochezi, kufanya maandamano bila kibali na uchochezi wa uasi.

Washitakiwa wote tisa wanatetewa na jopo la mawakili wa chama hicho, wakiongozwa na mwanasheria nguli nchini, Prof. Abdallah Safari.

Kwa mujibu wa rekodi zilizopo mahakamani, washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo, ni katibu mkuu wa Chadema, Dk. Vicenti Mashinji; naibu katibu mkuu Bara na mbunge wa Kibamba, John Mnyika; naibu katibu mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Katika orodha hiyo, wapo pia Halima James Mdee, mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Taifa la Chadema na mbunge wa Kawe; mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!